CCM KATA YA MAKUMBUSHO WAPIGWA MSASA JUU YA KATIBA.

 Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni wakiongoza wanachama kuapa(hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi kadi pya kwa wanachama wapya waliokaribishwa siku hiyo.Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam. 
 Viongozi wakiwaongoza wanachama kuapa.
 Baadhi ya viongozi wa matawi Kata ya Makumbusho wakienda sambamba na wanachama wapya kuapa mara baada ya kukabidhi kadi.
 Meza Kuu wakiongoza wanachama kuapa
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kata ya Makombusho tawi la CCM Mwinjuma.
 Wanachama wapya wa Kata ya Makumbusho Tawi la CCM Mwinjuma wakiapa mara baada ya kupokelewa uanachama kwa kukabidhiwa Kadi za CCM.
 Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Mwinyimkuu Sangaraza akiwapa Semina Wanachama wa Kata ya Makumbusho juu ya Katiba mpya.

 Mwenezi Sangaraza, akitoa Semina juu ya Katiba
 Mwenezi Sangaraza akitoa Semina
 Mwenezi Sangaraza akisisitiza jambo kwa wanachama juu ya katiba. 
 Semina ikiendelea. 
 Mwanachama mpya, Jane akikabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM.


 Mwanachama mpya wa CCM, Hidaya akikabidhiwa kadi ya uanachama.
 Mwanachama mpya wa Chama cha Mapinduzi, Rukia akipokea kadi.


Dar mabingwa Vishale Taifa.

 Machezaji wa vishale(Darts) wa klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa wameshika kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Friendz walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Bingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wa mchezo wa Vishale(Darts), Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi Wetu.
KLABU ya Friendz Wanaume yenye makazi yake Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo wa Vishale(Darts) Taifa  yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilichukuliwa na klabu ya Lugalo ambayo ilizawadiwa pia Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/=.
Upande wa Wanawake timu ya Friendz yenye makazi yake palepale Tiptop Manzese ilitwaa ubingwa wa Taifa na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 60,000/= wakati nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na klabu ya Kimanga ambao walizawadiwa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=.
Fainali za mashinadano ya mwaka huu zilikuwa na mchezo wa mmoja mmoja(Singles) na wawili wawili (Doubles) kwa Wanawake na Wanaume ambapo upande wa Doubles Wanaume, Jemes Mlai na Sylivanus Sylivester wote wa Ibukoni klabu waliiibuka mabingwa na hivyo kuzawadiwa Kikombe na Pesa Taslimu Shilingi 120,000/=, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu ya Jemes Enea na Nungwa Sadiloa wote wa Polisi Balax ambao walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 80,000/=.
Upande wa doubles Wanawake Subira Waziri na Happiness Modaha wote wa Klabu ya Ibukoni waliibuka mabingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/= wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Fabiola Namajojo na Veronica Sule ambao walizawadiowa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=
Upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanaume, Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo alitwaa ubingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi120,000/= wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Jemes Enea kutoka Klabu ya Polisi Balax ambaye alizawadiwa Kikombe na pesa taslimu 60,000/=.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi, aliwashukuru washiriki wote kwa moyo wa kujitoa kushiriki mashindano ya Kitaifa kutoka katika mikoa mitano kwa kujitegemea na pili aliwapongeza mabingwa waliofanikiwa na wale ambao hawakufanikiwa wakajipange kwa mwaka ujao.
Nae mwenyekiti wa Chama cha Vishale Taifa(TADA), Gesase Waigama aliwashukuru pia washiriki wote nakuwatakia safari njema za kurudi majumbani kwao pamoja na maandalizi mema kwa watakaoshiriki mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Mikoa iliyoshiriki mashindano ya Vishale Taifa mwaka huu ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.

Chocky aipasua Twanga.

 Mwimbaji wa nyimbo za mziki wa dansi, Ally Chocky (katikati) akitambulishwa kwa wapenzi na mashabiki wa mziki huo wakati onyesho maalum la utyambulisho kwa wanamuziki watatu, Ally Chocky, mcheza shoo, Super Nyamwela na mpiga kinanda, Victor Mkambi.Onyesho hilo lilifanyika jana katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Jijijini Dar es Salaam.Kulia ni Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Nyoni na msaidizi wake Kalala Junior.
 Chocky akiwapungia mkono mashabiki mara baada ya kutambulishwa rasmi.
 Mcheza shoo na Rais wa wacheza shoo, Super Nyamwela akifunguliwa kwenye beki ili atambulishwe rasmi wakayi wa onyesho maalum la utambulisho lililofanyika katika Ukumbi wa Mango Garden Dar es Salaam jana.
 Super Nyamwela akicheza wakati wa utambulisho wake katika Bendi ya Twanga Pepeta
 Choki akiimba mara baada ya utambulisho rasmi nyimbo ya "Usiyempenda kaja" utunzi wake yeye mwenyewe.

Na Mwandishi Wetu.
UJIO na utambulisho wa wanamuziki watatu ndani ya Bendi ya Twanga Pepeta umeleta mpasuko mkubwa uliopelekea kwa baadhi ya wanamuziki wakongwe na wenyeji wa bendi hiyo kutopanda kabisa jana wakati wa utambulisho rasmi wa Aliyekuwa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky pamoja na aliyekuwa kiongozi wa wacheza shoo wake, Super Nyamwela kurudi Twanga Pepeta.
Ally Chocky, Super Nyamwela na Mpiga Kinanda, Victor Mkambi wametambulishwa rasmi jana katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam na kushangiliwa na maelfu ya wapenzi na mashabiki wa mziki wa Dansi huku baadhi ya wanamuziki nguli na wenyeji wa Bendi hiyo kukosekana jukwaani.
Ripota wetu alizungumza na wahusika pamoja na viongozi wa bendi hiyo ambapo kiongozi wa bendi hiyo, Lwiza Nyoni hakupatikana kwenye simu lakini kiongozi msaidizi, Kalala Junior alipatikana na kukiri kuwa kunatatizo upande wa uongozi lakini hilo ni la ndani na kesho jumatatu wanakikao ambapo wanatarajia kulimaliza haswa la muimbaji Saleh Kupaza, Rama Pentagoni yeye alisimamishwa na anatarajia kumaliza adhabu hiyo Mai 3,2015 wakati Kibosho yeye kaihama Bendi na sasa yuko katika Bendi ya Diamond Platinam.
Ripota wetu pia alizungumza na wanamuziki kujiridhisha ambapo Saleh Kupaza alithibitisha kuwa kunatatizo ndani ya uongozi na haswa Kiongozi wa Bendi, Lwiza Nyoni ambaye alimkataza asipande kabisa jana wakati wa utambulisho wa wanamuziki hao kwa sababu ambayo alitaja kuwa hajafanya mazoezi ya nyimbo mpya ya Ally Chocky.Lakini Kupaza alisema “tatizo si hilo tu, mimi na Kiongozi Lwiza tumekuwa na matatizo muda sasa na msimamo wangu najua ndio unao nigharimu Kupaza, nimekuwa na msimamo daima kwenye maslahi na maendeleo ya bendi lakini Lwiza yuko kiofisi zaidi yaani hajali na badala yake naonekana mbaya siamini kama ujioa wa hawa wanamuziki umemuongezea kiburi cha kufikia kunikataza kupanda jukwaani hilo sijui ila ninatatizo nae”.
Ripota alimuuliza kama wanatatizo lolote na Chocky, ambapo alisema Kupaza, “mimi sina matatizo na Chocky wala ujio wa mwanamuziki mwenzangu yeyote nampenda Chocky hata yeye naamini ananipenda na ujio wake najua tutasonga mbele lakini alisisitiza tena sina tatizo na mtu yeyote zaidi ya kiongozi wangu Lwiza na hayajaanza jana matatizo hayo”.
Rama Pentagoni yeye alithibitisha kuwa anatumikia adhabu na Kibosho yeye tayari kishaihama rasmi bendi hiyo ya Twanga Pepeta yuko na Diamond kwa sasa.
Ripota wetu hakuishia hapo alipanda kwa Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Asha Baraka baada ya juhudi za Kiongozi wa Bendi, Lwiza Nyoni kutopatikana ambapo alisema swala hilo ni la kiutenjaji zaidi mwenye majibu sahihi ni Kiongozi wa Bendi Lwiza Nyoni ambaye kwa wakati huo alikuwa hapatikani katika simu yake ya mkononi.
Upande wa shoo kwa ujumla ilipendeza sana na ilikonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wengi wa muziki wa dansi waliojitokeza kushuhudia utambulisho huo.
Zaidi kilicho konga nyoyo za watu ni nyimbo mpa ya Ally Choki ya Usiyempenda kaja pamoja na nyimbo nyingi za zamani ambazo waliziimba pamoja enzi hizo Chocky akiwa Twanga walizikumbushia.                  


Choki akicheza sambamba na wacheza shoo wakati wa utambulisho huo Mango Garden Dar es Salaam jana.
 Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Nyoni akiimba wakati wa utambulisho wa wanamuziki hao Mango Garden jana.
Wacheza shoo wa kike wa bendi hiyo wakicheza wakati wa onyesho hilo.
 Chocky na Lwiza wakiimba kwa pamoja wakati wa onyeso hilo.
Wacheza shoo wakionyesha umahili wao.
 Kiongozi msaidizi wa bendi hiyo, Kalala Junior akiimba wakati wa onyesho hilo.
Wacheza shoo wakicheza. 
 Chocky na Rapa, Frenk Kabatano wakiimba wakati wa utambulisho huo.
 Wacheza shoo wakicheza. 
 Wacheza shoo wakicheza mbele ya mashabiki.

MASHINDANO YA DARTS TAIFA YAPAMBA MOTO DAR

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi(kushoto) akizindua rasmi mashindano ya mchezo wa Darts Taifa yanayofanyika Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam leo.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa(TADA), Gesase Waigama.
 Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi(kushoto) akizindua rasmi mashindano ya mchezo wa Darts Taifa yanayofanyika Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam. 
 Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam
 Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofunguliwa  Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.
Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa  kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.
Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha haya yote.
Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee  wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.
Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama salimini.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja), Doubles(wawili wawili) na Timu.
Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.