Friday, February 24, 2012

EXTRA BONGO WAONGEZA NGUVU TENA.

Kikosi cha mbele kilichobomolewa Stone Mayasika

a Michael Machellah
MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky ameibomoa safu ya

mbele ya Bendi ya Stone Mayasika.

Akizungumza na mtandao huu Chocky alijijitea kuwa si yeye aliyefanya hivyo

bali ni wacheza shoo wenyewe wameamua kuihama kwa mapenzi yao na maslahi

yao binafsi.

Wakizungumza na mtandao huu walisema ukweli kuwa Extra Bongo iko

juu,kuanzia kwenye jina huwezi kuilinganisha na Stone Mayasika,pili Extra

Bongo ina wapenzi wengi ukilinganisha na Stone Mayasika,tatu ni bendi

inayoongoza kwa sasa katika Bendi za muziki wa Dansi na mwisho ni maslahi

ndio yaliyowatoa Stone Mayasika kwenda Extra Bongo.

Kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela alisema ni kweli wacheza shoo hao

wapo na tayari wameshaanza kucheza wakati wakiwa kambini kufundishwa

yaliyopo na yanayojili Extra Bongo.

Extra Bongo leo watakuwa viwanja vya Kijichi,kesho jumamosi ni katika

Uwanja wa Nyumbani Meeda Sinza Dar es Salaam na jumapili ni Dar Live

0 comments:

Post a Comment