Tuesday, October 9, 2012Kampuni ya Bigright Promotions imeipongeza oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini(TPBO) kwa kumteua Bw. Masoud Sinani kuwa makamu wa rais wake.
Bw. sinani mwenye stashahada ya biashara aliyoichukulia katika chuo cha salsbury cha nchini  Uingereza ni mdau wa karibu wa michezo,mhamasishaji na mratibu wa michezo mkoani Mtwara.
TPBO katika kujipanga vizuri imeonelea ni bora kuimarisha safu ya uongozi mikoani,kwa hiyo ofisi ya makamu wa rais yaweza kuwa Mtwara,
TPBO ambayo imejijenga vema nchini na kuendeleza mchezo wa ngumi kwa kuwapa kipaumbele mabondia wa mikoani katika kunyanyua vipaji vyao na kuamsha mchezo wa ngumi pale ambapo umelala na watu kudhani hakuna mabondia eneo hilo kumbe wapo.
Juu ya pongezi hizo Bigright promotion kupitia mkurugenzi wake Ibrahim Kamwe imeahidi kuiunga mkono TPBO katika kuendeleza mchezo wa ngumi na kusaidiana nayo kwa nguvu zote katika utendaji.
Wakati huohuo TPBO yenyewe imepanga kukutana na viongozi wake,marefa na majaji makao makuu ya ofisi hiyo,tarehe 10/10/2012 katika semina fupi na mkutano utakaozungumzia mpambano wa bingwa wa taifa Thomas Mashali atakaezipiga na mganda Med Sebyala tarehe 14/10/2012 kugombania ubingwa wa Afrika mashariki na kati

0 comments:

Post a Comment