Monday, October 8, 2012


 Mwenyekiti mpya wa Chama cha Darts Tanzania(TADA), Gesase  Waigama( kushoto) na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
CHAMA Cha Darts Tanzania(TADA), kimefanya uchaguzi rasmi  na kuwachagua viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa miaka mitatu baada ya kukaa na Uongozi wa kuteuliwa kukaimu madaraka kwa muda.
TADA ilifanya uchaguzi kupitia wajumbe wake wa kamati kuu kutoka katika mikoa yote ya Tanzania chini ya usimamizi wa  Wajumbe kutoka Baraza la Michezo Tanzania na kuwasimika, Gesase Waigama kutoka Klabu ya Ibukoni Tabata Segerea ya  Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa kuchaguliwa kisheria atakaye iongoza DATA kwa miaka mitatu.
Makamu mwenyekiti alichaguliwa David Msabi kutoka Klabu ya Mzinga Morogoro,Katibu Mkuu wa Tada alichaguliwa Kale Mgonja kutoka Klabu ya Kashudu ya Magomeni Dar es Salaam ambapo makamu wake alichaguliwa Tareto Kitali kutoka Klabu ya Magereza Moshi.Katibu Mwenezi wa TADA alichaguliwa Ignas Bwangaya kutoka Klabu ya Katumba Kinondoni Dar es Salaam na Mwekahazina wa chama hicho alichaguliwa Harrod Mono kutoka Klabu ya Kashudu ya Dar es Salaam.
Upande wa Wajumbe wa kiume walichakuliwa, George Kassama kutoka Klabu ya Safari ya MKOANI Kagera Kanda ya Ziwa,Ramadhani Simba kutoka Magereza Moshi,Adelade Chikoma kutoka Polisi Mbeya,Andrew Samo kutoka Pwani,Eakimu Rwisigalo kutoka Pwani na Dokta Mwiru kuoka Kanda ya Kati Dodoma.
Wajumbe wakina mama walichaguliwa, Subira Waziri kutoka Dar es Salaam,Josephine Lamuyani kutoka Arusha,Fabila Namajojo Kutoka Morogoro,Anna Mwakabonga kutoka Mbeya na Safina Msuya kutoka Magereza Moshi.
Mwenyekiti mpya wa miaka mitatu ijayo, Gesase Waigama aliwashukuru wasimamizi kutoka Baraza la michezo Tanzania  kwa usimamizi mzuri ambao haukuwa na malalamiko na kuwataka wajumbe wote waliogombea na kuchaguliwa kuwajibika kufanya kazi kwa nafasi zao kwa kufuata Katiba ya chama  ili kuiendeleza Darts Tanzania na pia aliwashukuru wajumbe wote walioshiriki uchaguzi na kuwachagua na wale ambao hawakuchaguliwa alisema atatoa ushilikiano kwao katika kuendeleza chama na mchezo na kuwaomba wagombee tena awamu nyingine.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo ambaye anadhamini Darts aliwapongeza Viongozi waliochaguliwa ambao wengi wao ni wale walikuwa kwenye uongozi wa kuteuliwa na pia aliwapongeza wajumbe waliowachagulia kwani hicho ni kipimo tosha cha kudhihirisha kuwa wanafanya kazi vizuri na ndio maana wamechaguliwa hivyo atatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mchezo wa Dars unaenea nchini kote na kurudi kwenye thamani yake.

0 comments:

Post a Comment