Monday, October 15, 2012


Baadhi ya waisilamu wa kijiji cha Dogo Dawa wakikimbia baada ya kushambuliwa wakati wakitoka msikitini.
Wakuu wa Nigeria wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha wamewauwa watu kama 20 katika shambulio lilofanywa alfajiri kwenye kijiji cha Dogo Dawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi.
Waliouwawa wengi walikuwa wakitoka msikitini. Washambuliaji walifyatua risasi na kuwapiga visu waliokuwako na tena walimuuwa mzee wa jamii nyumbani kwake.
 
Afisa wa habari wa jimbo hilo, Saidu Adamu, aliiambia BBC kwamba gengi la majambazi wa jimbo hilo walifanya mauaji hayo.
Alisema shambulio hilo ni la kulipiza hatua iliyochukuliwa na wanakijiji cha Dogo Dawa ya kuunda kikosi cha wanamgambo wao wenyewe kuwatimua majambazi hao ambao wamekuwa tishio kijijini.

0 comments:

Post a Comment