Monday, October 8, 2012


 Mkufunzi wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji, ally Seleman akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Wiki hiyo inayoanza tarehe 10-13 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
Mratibu wa Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji, Geofrey Kivamba akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.  
 Na Lucy Ngowi

WIKI ya Huduma za Fedha na Uwekezaji kwa wadau mbalimbali  inatarajiwa kuanza Oktoba 10-13 jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa wiki hiyo, Geofrey Kibamba alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku hiyo ambayo itakuwa siku tatu.

Alisema lengo la wiki hiyo ni kutoa elimu  kuhusu matumizi bora ya taasisi mbalimbali za kifedha.

Kibamba alisema uelewa mdogo wa elimu kuhusu huduma za kifedha umekuwa chanzo cha wengi kushindwa kuelewa jinsi ya kutumia taasisi hizo ambazo ni muhimu katika maendeleo.

Kwa upande wake, Mtaalam elekezi wa huduma za maendeleo ya jamii kutoka ‘Tanzania Consumer Advocacy Society’, Abdul Ally alisema zaidi ya asilimia 54 ya watanzania hawatumia huduma rasmi za kifedha.

“Asilimia 9 ndio wanaotumia huduma rasmi. Hii inaonyesha jinsi gani tanzania tupo nyuma,” alisema.

Alisema utafiti huo ulifanywa 2006 hadi 2009 na kubaini hayo.

0 comments:

Post a Comment