Friday, November 16, 2012
Picha za msanii wa Bongo flava Ney wa mitego mwenye maneno ya shombo kwa wasanii wenzake kuhusu ukahaba wa wasanii wa bongo movie zimenaswa mtandaoni akiwa amepozi kimahaba na msanii wa bongo movie Nisha.
Mtu mzima True boy akidendeka ...... mistari chaliiii..!!
Ney wa mitego ameonaka kama mtu ambae anafichua maovu mengi ya tabia za ukahaba wa wasanii wa tasnia ya filamu angali yeye ndiye mteja mkuu wa makahaba hao kwa mujibu wa kauli yake kuwa makahaba wenye viwango wako bongo movie.
Taswira hii itamuweka Ney katika hali ngumu kwani hatofautiani sana na wale aliowapaka matope kwani anaruka mkojo na kukanyaga kinyesi au alikuwa anasema tu ili kujipatia umaarufu kitu ambacho kimeaacha midomo wazi wadau wa muziki na filamu.
Ney na Nisha wamewahi kukanusha mara kadhaa kuhusu uhusiano wao na leo mambo yamekuwa hadharani...mmhh patamu hapo.
Hebu tuone nini kitajili baada ya Ney kutoa kauli yake kuhusu picha hizi ambazo zitazua gumzo kubwa kama si kuonekana mnafiki au ni triki za kibiashara tu.
 True boy kibwaya chako safari hii...!

0 comments:

Post a Comment