Tuesday, February 5, 2013Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiteta na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika katika viwanja vya Bunge leo, baada ya hoja yake binafsi kukataliwa Bungeni.PICHA ZOTE /MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa ufafanuzi hali iliyotokea Bungeni leo.

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (kushoto) akifurahia jambo na William Ngeleja (Sengerema), katika viwanja vya Bunge baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda (hayupo pichani) kuahirisha kikao hadi kesho.

Mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo (kushoto), pamoja na Said Arfi (Mpanda Mjini)wakifuatilia hoja mbalimbali Bungeni leo Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Stella Manyanya (Viti maalumu) kuhusu yaliojiri Bungeni leo.

Waziri wa  Viwanda na Biashara,  Dkt. Abdalla Kigoda (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Wazri wa afya na Ustawi wa  Jamii, Dkt Seif Rashid katika viwanja vya  Bunge leo baada ya kuahirishwa mkutano wa kumi, kikao cha sita.

0 comments:

Post a Comment