Friday, February 15, 2013


Mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius wa Afrika Kusini ashikiliwa na Polisi!kwa shutuma za kumuua Mpenzi wake !

WAKATI wengine wanasherekea siku ya wapendanao duniani ! lakini kwa mwanamichezo Oscar Pistorius imekua kinyume ! badala ya furaha ni msiba! Asubuhi na mapema alhamisi 14/02/2013 huko Pretoria, Afrika kusini Polisi walitia mkononi mwanamichezo nyota aliyejipatia umarufu katika michezo ya Olympic Bw.Oscar Pistorius (26),ametiwa nguvuni ana polisi wa nchi hiyo kwa madai ya kumuua mpenzi wake model Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi! Inasemekana alhamisi 14/02/2013 asubuhi milio ya risasi ilisikika nyumbani kwa mwanamichezo huyo mjini Pretoria na polisi walipofika walimkuta mpenzi wa mwanamichezo huyo Bi. Reeva Steenkamp (30) ambae pia ni model ameshauwawa. Polisi wa Afrika kusini wanategemea kumfikisha mahakamani bw.Oscar Pistorius (26) kwa mashtaka ya mauaji siku ya ijumaa ya 15/02/2013.  

0 comments:

Post a Comment