Tuesday, February 5, 2013
Odama mwigizaji wa filamu Swahiliwood.KILA jambo lina uzuri wake na kwa wasiolewa wanaweza kuleta tafsiri tofauti na wahusika au mhusika, mwaka huu mwanadada Jennifer Kyaka ‘Odama’ anayefanya vema katika tasnia ya filamu Swahiliwood katika kuimalisha kampuni yake na kujiongezea kipato, kampuni yake ya J- Film 4 Life, alitengeneza kalenda iliyosheheni picha za wasanii wa filamu, maneno yakazuka.

.


Kalenda inayolalamikiwa kumtosa Mussa Banzi.Filamu ya Unbroken Promise aliyoigiza Mussa Banzi na Odama.Baadhi ya wasanii walioigiza na Odama akiwa katika kundi la White Elephant linaloongozwa na Mussa Banzi ambalo ndilo hasa lilomtoa Odama lakini wameshangaa kwa mwanadada huyo ametengeneza kalenda iliyoweka picha za wasanii wote lakini hakuweka picha ya Bosi wake wa zamani Mussa Banzi pengine wenye wanahisi bila Mussa Banzi Odama asingekuwepo katika tasnia ya filamu.

Baada ya kusikia minong,ono hiyo FC ilifuatilia suala hili kwa undani na kubaini kweli kutokuwepo kwa picha ya Mussa Banzi katika picha zilizoremba kalenda hiyo ikiwa ni mmoja kati ya watu wenye mchango mkubwa kwa msanii huyo kufanikiwa katika tasnia ya filamu Bongo, FC iliongea na Odama.
.


Mussa Banzi bosi wake wa zamani wa Odama.Odama akiwa katika pozi.

0 comments:

Post a Comment