Thursday, February 28, 2013
 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
 Jaji Mkuu wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa, Joseph Migunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
.
Dar es Salaam, Alhamisi 28 February 2013: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imefunga  rasmi zoezi fomu za ushiriki wa programu ya wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema kwamba zoezi la fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu huu tumelifunga rasmi leo. Baada ya hapa fomu hizo zitakusanywa kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

0 comments:

Post a Comment