Thursday, February 7, 2013

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mwisho wa kurejesha fomu za programuya Safari Lager Wezeshwa.Kulia ni Mratibu wa Programu hiyo, Lawrence Andrew.
Na Mwandishi wetu.
 KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu za ushiriki wa programu ya wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema kwamba fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu huu zinaendelea kupokelewa sasa hivi na zoezi hili litakamilika rasmi Ijumaa tarehe 01 March 2013. Baada ya hapo fomu hizi zitakusanywa kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi. Bwana Shelukindo alisema, “Tunawakumbusha wajasiriamali wote ambao wangependa kushiriki kwenye programu msimu huu kwamba fomu zinapatikana katika ofisi za TBL mikoani kote, maduka ya wauzaji wa jumla wa bidhaa za TBL na pia zinapatikana katika website ya programu ya Wezeshwa ambayo niwww.wezeshwa.co.tz”. 
Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Alisema, “Upatikanaji wa fomu hizi ndio mwanzo rasmi wa safari kuelekea uwezeshaji wa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa msimu huu. Safari Lager inatoa fursa kwa mara ya pili,  inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza fomu za ushiriki na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.  
Naye Bwana Joseph Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hiialisema kwamba sifa za kushiriki ni sawasawa na ilivyokuwa msimu uliopita. Alieleza kwamba wajasiriamali watakaojitokeza kushiriki wanapaswa kuwa na sifa kuu nne; wawe wachapakazi hodari, wawe wanamiliki biashara binafsi ambazo ni halali, wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na wawe na nia ya kukuza biashara zao ili ziweze kuwasaidia wao na jamii inayowazunguka. Bwana Migunda alieleza kwamba vigezo vinavyotumika kupata watakaofaulu ni pamoja na kufuata vizuri maelekezo ya ushiriki, kuwa na wazo ambalo ni la ubunifu zaidi, kuwa na biashara ambayo inasaidia jamii inayoizunguka biashara hii nk. Alimaliza kwa kusema kwamba “Natoa wito kwa wajasiriamali kote Tanzania wajiandae vizuri, watayarishe nakala sahihi za hati za biashara zao, wasome na kujaza vizuri kwa usahihi fomu za ushiriki na wawe na uhakika kabisa kwamba TAPBDS kama waratibu wa “Safari Lager Wezeshwa” tutahakikisha vigezo vilivyowekwa vinatumika vizuri katika kumpata mshindi wa kweli”. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara zao. 
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.

0 comments:

Post a Comment