Tuesday, February 5, 2013

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia) akikata nyama kuashilia uzinduzi wa shindano la Safari Lager Nyama Choma linalotammbulika kwa jina la “Safari Lager Nyama Choma Competition 2013”lililozinduliwa TBL jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji Mkuu wa shindano hilo, Douglass Sakibu.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Nyama Choma 2013 kwa Bar mbalimbali lijlikanalo kama ‘’Safari Lager Nyama Choma Competition 2013” liliofanyika TBL jijini Dar es Salaam .Kulia ni Jaji Mkuu wa shindano hilo, Douglass Sakibu na mratibu wa Shindano hilo, Peter Zacharia.
 
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi shindano lauchomaji nyama kwa baa mbalimbali lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2013”. 
Shindano hili linalofanyika kila mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya sita mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar Es Salaam. Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo. Kwa mwaka huu walaji wa nyama choma watatakiwa kupigia baa zao kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda namba0763 514 514. Ujumbe huu utatozwa gharama za kawaida za kutuma ujumbe, hakutakuwa na makato ya ziada kwa mitandao ya simu. Baa tano zitakazopata kura nyingi zaidi zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakaloandaliwa katika mikoa yote, washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu. Zaidi ya shilingi milioni ishirini na sita zitatolewa kama zawadi kwa washindi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, meneja wa bia ya Safari Lager bwana Oscar Shelukindo alisema kwamba, “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma. Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Bwana Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.  
Kiongozi wa jopo la majaji ambao ni wataalamu maarufu nchini katika tasnia hii, bwana Douglass Sakibu alielezea kwamba majaji wataangalia kwa makini sana vigezo mbalimbali katika utayarishaji wa nyama choma. Alitaja baadhi ya vigezo hivyo kwamba ni usafi, vifaa vya kufanyia kazi, joto maalum la uchomaji nyama nk. Bwana Sakibu aliendelea kusema kwamba, “Tunawaomba bar zote kujitokeza katika semina ya utangulizi tutakayofanya katika mikoa yote inayoshiriki, Katika semina hii tutakumbushana mambo muhimu ya kuzingatia ili kumpa mteja nyama choma bora zaidi, muda wote anapoihitaji”. 
Naye bwana Peter Zacharia, wa kampuni ya Integrated Communications inayoratibu shindano la Safari Lager Nyama Choma alisema, “Tunaomba wachoma nyama kujitokeza kwenye semina hizi, mafunzo yatatolewa bure. Seminar kwa baa za wilaya ya Temeke itafanyika Imasco Bar uwanja wa Taifa Jumatatu tarehe 11 February. Baa za wilaya ya Ilala seminar itafanyika Jumanne tarehe 12 February katika baa ya Beriego Ilala Bungoni. Kwa wilaya ya Kinondoni semina itafanyika Jumatano tarehe 13 February katika baa ya Meeda Sinza”. Bwana Peter alitaja pia tarehe za semina za mikoani kama ifuatavyo; Baa za mkoa wa Mbeya, Ijumaa tarehe 8 February, baa za mkoa wa Mwanza Ijumaa tarehe 22 February, baa za mkoa wa Arusha Jumatano tarehe 27 February na baa za mkoa wa Kilimanjaro Alhamisi tarehe 28 February. 
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lagertutaendeleakujitahidikuhakikishawatejawetuwanapatahuduma bora yanyamachoma pale wanapoihitaji. Tunawaombasanawashirikikutumiavizurielimunauzoefuwanaopatailikuongezauborawautayarishajiwanyamachomakwawatejawetu. MashindanohayayaSafari Lager NyamaChomayatakosamaanasahihiendapowachomanyamawatakuwawanashirikikwalengo la kujipatiamanufaabinafsinakusahauyaleyotewaliyojifunzahadimwakamwingine”.Shindalo la mwakahuulinaongozwanakibwagizo…. Bila Safari Lager, NyamaChomahaijakamilika!.

0 comments:

Post a Comment