Wednesday, February 13, 2013
Mdau Selemani Katto ameshangazwa na kusikitishwa na maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi kwa kumuondoa Malinzi kwa kigezo cha uzoefu.
Mdau Salum Mkemi ametoa hoja ya mwamba Malinzi ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera vipi akose sifa ya kuwania nafasi ya urais wakati sifa za kuwania Urais ni zilezile. Lakini pia amekumbusha kampeni za uchaguzi wa CCM mwaka 2010 ambapo kulikuwa na bifu la Murtaza Mangungu na Juma Matandika ambaye ni ndugu yake na Malinzi hivyo wanabifu la tangu wakati huo vilevile kuna uswahiba wa tangu Temeke na Kwamba mweyekiti wa kamati ya rufaa ya uchaguzi inaongwa na Iddi Mtingijola wakati wao ni marafiki tangu ofisini wakati huo Mtingijola alikuwa bosi wa Nyamlani hivyo kuna kulindana.
Kutoka kushoto ni mdau Saidi Bakari, Ayubu Nyenzi na Dossi Matola.
Salum Mkemi akisisitiza madai yake ya kupinga maamuzi ya rufaa ya uchaguzi wa TFF.
Meza ya wadau wakipinga maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF chini ya Iddi Mtingijola.
Mdau Kaisi Edwin naye anasema kanuni mpya zimetengenezwa kwa ajili ya kuwaengua baadhi ya wagombea hivyo watasimamisha uchaguzi mahakamani na pia wanataka mahakama ya michezo CAS kuingilia kati juu ya hilo ni bora kufungiwa na FIFA. Anahoji kwa nini TFF kuna akaunti mbili jambo ambalo limemtia shaka ndio maana watu wanapingwa kuingia katika system ya mpira wa Tanzania wanaogopa maovu yatabainika.

0 comments:

Post a Comment