Saturday, March 2, 2013
LONDON, England

“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi nami nakuhakikishia niko tayari kwa lolote. Kasi yangu na ujuzi nilionao ulingoni, nguvu zake na uzoefu alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia"
BONDIA Amir Khan amekiri kuisubiri kwa hamu Aprili 27, siku ambayo atarejea ulingoni kumvaa Julio Diaz kwenye ukumbi wa Motorpoint Arena.
Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kwa Khan katika ardhi ya Uingereza, tangu alipokubali kichapo kutoka kwa Paul McCloskey jijini Manchester mwaka 2011.
Na Khan, 26 amethibitisha alivyoupania mpambano huo kurejesha heshima yake iliyotoweka ulingoni – huku akisema: “Aprili 27 unaelekea utakuwa usiku maalum.
“Imeshapita miaka miwili sasa tangu pambano langu la mwisho katika ardhi ya nyumbani na sitasubiri kupanda tena ulingoni na kufanya vitu adimu mbele ya mashabiki wangu.
“Diaz ni bingwa wa zamani wa Dunia na ni mpinzani hatari mno ulingoni. Najua atakuja ulingoni akiwa na silaha kamili za maangamizi nami nakuhakikishia niko tayari kwa lolote.
“Kasi yangu na ujuzi nilionao ulingoni, nguvu zake na uzoefu alionao, vinalifanya hilo liwe moja ya mapambano makali unayopaswa kuyashuhudia.
“Yeye anaweza kuwa na amawazo kama waliyonayo wengine, nina imani kuwa marejeo yangu katika ardhi ya Uingereza yatakuwa ya mafanikio makubwa ulingoni.”
Diaz, 33, hajawahi kupigana kwa raundi 12 tangu alipopokwa mkanda wa IBF – uzani wa  ‘light’ alipoumana na Juan Diaz mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment