Saturday, March 2, 2013
Bondia Aliphonce Mchumiatumbo (kushoto) akioneshana umwamba na Josephe Marwa, Dar es salaam , baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa uzito wa juu utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa  march 2 jumamosi PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Aliphonce Mchumiatumbo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa uzito wa juu na Josephe Marwa utakaofanyika jumamosi ya  March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa
Josephe Marwa katikati akiwa na baadhi ya mabondia

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Japhert Kaseba kulia,Josepher Marwa na Aliphonce Mchumiatumbo wa pili kushoto baada ya kupama uzito kwa ajili ya mpambano wa March 2
Bondia Maneno Osward akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Japhert Kaseba utakaofanyika March 2 katika kumbi wa DDC Magomeni Kondoa kulia ni Katibu wa PST Antony Luta ambaye alikua anasimamia zoezi la upimaji uzito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Japhert Kaseba kulia,Josepher Marwa na Aliphonce Mchumiatumbo wa pili kushoto baada ya kupama uzito kwa ajili ya mpambano wa March 2

Mabondia Japhert Kaseba kushoto akitunishiana misuri na Maneno Osward baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa utakaofanyika DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam March 2 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comNa Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo

Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini 

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

0 comments:

Post a Comment