Saturday, March 2, 2013

.
Msijitutumue na kuwakoga mliowashinda kwenye uchaguzi.
Sasa kazi muhimu ya UVCCM ni moja tu, kuifanya CCM ishinde chaguzi zote.

NA BASHIR NKOROMO.

MOROGOROMWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Hamis Juma Sadifa amesema baada ya uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana, sasa kazi iliyopo mbele ya UVCCM ni kuhakikisha CCM ni inaimarika zaidi na kushinda chaguzi zote.

Amesema baada ya uchaguzi huo na uteuzi wa Viongozi wa Baraza Kuu, wajibu walionao viongozi wa Jumuia hiyo sasa ni kujishusha chini  na kuacha kabisa tabia ya kujitutumua na kuwagoga waliowashinda kwenye uchaguzi ikiwa ni njia mojawapo ya kuvunja makundi ndani ya jumuia hiyo.

Sadifa alisema hayo, Februari 28, mwaka huu, wakati akizungumza na Baraza Kuu la UVCCM mkoa wa Morogoro, alipowasili kwa ajili ya ziara ya siku tatu mkoani humo ambayo ni ya kwanza kufanya nchini tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo.

"Baada ya uchaguzi kumalizika na kukamilisha uteuzi wa wajumbe wa Baraza letu kuu, sasa kazi iliyobaki mbele ya ni kuhakikisha CCM inakuwa imara na kushinda chaguzi zote zinazokuja. Wale tuliochaguliwa sasa tujishushe kwa wanachama wetu, na kuacha kabisa tabia tuliyonayo baadhi yetu ya kujitutumua na kuwakoga tuliowashinda, tabia hizo hazina faida na ni sumu kabisa kwa uhai wa Jumuia na Chama chetu", alisema.

"Tabia hiii tuiache kabisa, ni sumu inayoendeleza makundi yaliyotokana na uchaguzi, kuendelea kwake ndiko kumekuwa kukisababisha CCM kushindwa katika chaguzi mbalimbali hata katika maeneo ambayo wapinzani wala hawajai mkononi, eeh, wakipata kura zao kidogo na za sisi wenyewe tunaovurugana wanashinda!" alisema.

Alisema, ni wajibu wa viongozi walipata nyadhifa, kuwabembeleza waliowashinda ili kuwaleta karuibu yao, badala ya kuwananga na hivyo kusababisha kujenga mpasuko ndani ya Jumuia hiyo ambao alisema siyo lazima kuwepo kama busara hiyo inatumika.

"Wewe ukishakuwa kiongozi, jitahishi kutumia kila mbinu kuhakikisha yule uliyemshinda au ambaye hakukuunga mkono wakati unatafuta ushindi unakuwa karibu naye kiasi cha kujenga urafiki wa kumfanya akuamini kwamba wewe ni muungwana, hivyo ndivyo siasa inavyotakiwa kufanywa", alisema Sadifa na kuongeza;

"Unajaribu kwa mara ya kwanza kumvuta, ukishindwa unajaribu tena hata mara ya pili hadi ya tatu, kama naye ni muungwana lazima ataondoa kinyongo, na kama ukiona haelekei kuwa kuondoa kinyongo mwache, lakini usimchukie kabisa maana kama hakukuunga mkono wakati huu ipo siku atakuunga mkono kwa jambo jingine".

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM, yupo pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa wa Jumuia hiyo wakiwemo Katibu Mkuu, Martine Shigella na Naibu Katibu Mkuu Mfaume Kizigo na makada wawili wa aliohamia CCM hivi karibuni wakitoka Chadema, Mwampamba na 

Katika siku tatu za ziara hiyo viongozi hao watatakwanyika wilaya karibu zote za mkoa wa Morogoro na kushambulia kila kona kuimarisha uhai wa Chama.

0 comments:

Post a Comment