Saturday, March 2, 2013
Usain Bolt
PARIS, Ufaransa

'Kuwa pamoja na Bolt, tunajua kwamba itakuwa rahisi kwetu kuujaza uwanja wa Stade de France'
BINADAMU anayeshikilia rekodi ya kasi zaidio duniani, Usain Bolt anatarajia kulipwa kiasi cha pauni 10,000 kwa sekunde moja – wakati atakaposhiriki kukimbia mbio za nmita 200 za Paris Diamond League kiangazi hiki.
Bolt mshindi mara tatu wa mashindano ya Olimpiki, anatarajia kulipwa pauni 200,000 wakati atakapokuwa akijiandaa kwa ajili ya Michuano ya Dunia Agosti mwaka huu kwa itakayofanyika jijini hapa Julai 6.
Waratibu wa Mbio za London Grand Prix Julai 27 wana matumaini ya kumvutia Bolt raia wa Jamaica, baada ya kuondolewa kwa sheria tata za makato ya kodi kwa wageni.
Tayari Bolt amekubali kushiriki mashindano mengine mawili mwaka huu, mbio za mita 150 zitakazorindima kwenye fukwe za Copacabana nchini Brazil hapo Machi 31 na zile za mita 200 za Oslo's Bislett Games zitakachukua nafasi hapo Juni 13.
Licha ya kitita kikubwa itakachotumia kumlipa Bolt katika mbio zake, Mkurugenzi wa Paris Diamond League, Laurent Boquillet amesisitiza watatumia vema pesa za uratibu.
'Kuwa pamoja na Bolt, tunajua kwamba itakuwa rahisi kwetu kuujaza uwanja wa Stade de France,' alisema akionesha kukiamini asemacho.
The Sun

0 comments:

Post a Comment