Thursday, March 7, 2013
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wa pili kulia akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Kushoto ni wanamuziki Shabani Dede, Hassani Moshi,Zahoro Bangwe na Amri Said ' Dongo'
Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakionyesha umahiri wao wa kupuliza 'midomo ya bata' wakati wa bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. kutoka kushoto ni Shabani Lendi, Hamisi Mnyepe na Roman Mng'ande
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, kulia akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma. kushoto ni Othumani Kambi, Shabani Dede na Hassani Moshi picha
Kwa hisani ya Sufianimafoto blog.

0 comments:

Post a Comment