Sunday, December 8, 2013Kais Mussa Kais (Mzee wa Fitina).
Bendi inayokuja kwa kasi ya ajabu Supershine Modern Taarabu imeweza kuingia katika tamasha la mitikisiko ya pwani 2013 ambalo litafanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala siku ya jumamosi tarehe 14. 

Supershine imeonesha ukomavu mkubwa baada ya kuzipiku bendi zingine kubwa ambazo hazikufanikiwa kuingia katika tamasha hilo.
Bendi ambazo hazikuchagulia ni pamoja na Coast Modern Taarabu, Kings Modern Taarabu, T. Moto na nyinginezo...

Bendi zilizoingia top 5 ni:
Supershine Modern Taarabu, 
Jahazi Modern Taarabu, 
Five Stars, 
East African Melody na Mashauzi Classic

Akizungumza na blog hii ya Taarabu Zetu meneja wa Supershine Kais Mussa Kais ukipenda muite "Mzee wa Fitina" alisema, mwaka huu kulikuwa na ushindani mkubwa sana mchujo ulifanyika zaidi ya mara 2 katika kutafuta ni bendi ipi ya kushiriki tamasha la mwaka huu, lakini kikubwa nawashukuru sana wadau kwa kutuchagua kwa kura zao nasi tunawaahidi burudani nzuri.

0 comments:

Post a Comment