Wednesday, January 15, 2014

Bondia Pendo Njau, pichani
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi na mateke ‘Kick Boxing’, Pendo Njau, amesema kwamba Tanzania ina uhaba wa mabondia hivyo ni kazi kubwa kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi.

.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Pendo alisema kwamba uhaba huo ni tatizo kubwa, hivyo kuna haja ya maabinti wanaopenda ngumi kujitokeza kwa wingi ili kuongeza chachu ya masumbwi.
 
Alisema wanaume wamekuwa wengi sana huku wanawake wakiwa wachache, ikiwa ni hatua inayosababishwa na mfumo wetu na imani ya wanawake kuwa wao hawapaswi kufanya kazi ngumu.
 
“Mwanamke hawezi kupigana na mwanaume, hivyo sisi ambao tunacheza ngumi tunapokuwa wachache hatuwezi kufika mbali kwasababu hatuna nafasi ya kufunzana na kupandisha viwango vyetu.
“Huu ni wakati muafaka kwetu sisi wanawake kuzidi kujitokeza kwa wingi kujifunza ngumi ili tutafute ajira kwa mtindo huo kwasababu ni sehemu inayoweza kuajiri watu wengi,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Pendo, mabinti wengi watakavyoingia katika mchezo wa masumbwi utaongeza tija kuutangaza ndani na nje nchi.

0 comments:

Post a Comment