Sunday, January 19, 2014 CHA KUOKOTA SIO CHA KUIBA.Edward Lowassa, ehemaliger Premierminister Tansanias, im Interview mit der DW
DW/ Aboubakar Liongo
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa. 


Kwa utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU KWELIKWELI sio masihara.
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.

Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu". 


Hatutaki kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu,fitna,kuchongeana,uchu wa madaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA. kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandikakwa facts and figures kama anavyosemaga Prof.Muhongo. 

1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
Nianze na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa BRN.Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI,MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaan we want things to happen now. 


Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweli LOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.


Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi. 

HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.  
Naamini huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye point ya tatu. 


2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.

Jamani Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye dawati,alivyoshusha ada n.k Tusisahau kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu. 


Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie. 


Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL. 


3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS) 
Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".


Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.

Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges. 


Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT. 


A FOCUSED MAN 4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua LOwassa ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga chini.


Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi itakayotukomboa Tanzania. 


Na ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA ....(nitamuongelea wakati mwingine) 

5.LOWASSA ANASIKILIZIKA,ANAFUATILIA,SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
Hii ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha nyuma. 

Rais anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa kiongozi anataka hili lifanyike.

LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili. 
KUTOKA KWENYE UKURASA ZA MTANDAO WA KIJAMII Lauden Mwambona

6 comments:

Anonymous said...

hakika ndiye kiongozi ambaye ana kila sifa ya kuwa Rais wetu kutokana na uwajibikaji wake kitu ambacho kilichopelekea hata kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hivi karibuni bungeni!

Anonymous said...

Ni mtu anaeijua nchi hivyo anajua vipaumbele. Sio mtu wa nadhalia. Ni mchapa kazi na mpanga kazi na anajua kusimamia.

Anonymous said...

Tusikubali uzushi dhidi ya lowassa, mahakama zipo mbona hawampeleki, amewazidi kwa kila kitu kizuri hivyo wamemua kutengeneza uzushi na hivyo hawana kitu cha ku- prove beyond reasonable doubt kama sharia inavyo taka. Lowassa ndiye hatima ya maendeleo yetu kafanya mazuri mengi sote tunajua. Epukeni hao wanaojifanya mitume. piteni kwenye majimbo yao ya ubunge ni wala rushwa wakubwa.

Anonymous said...

Asante kwa ufafanuzi. Itasaidia wengi waliokuwa kama vifaranga walioachwa baada ya mama Yao kuliwa na Mwewe. Kashfa ya Richmond ilimharibia sana Mkuu- kwa jinsi tulivyomuona msaliti, wa kizazi chetu na Taifa hili. Baada ya kigundua zilikuwa fitina, nilimwonea huruma sana, nikagundua binadamu wengine ni viumbe wa ajabu, wanaweza kusababisha na kutoa hata uhaI wa mtu for selfish reasons, to satisfy their egos. Nimempenda Mmarekani (Pres. Barack Obama) kuja mwenyewe hadi TZ kumsafisha Mzee wetu, Mheshimiwa Edward Lowassa. Sifa zake kama ulivyozitaja, na anazo pia zile za kikwao, Kimasai. Hata iwe usiku, akiamua jambo lake ni hadi litimie, ana subira, hana papara, utatukana matusi yote,Utampaka matope yote, pengine utachimba shimo umtupie taka taka mpaka juu, he will surely shove all of it off, atatoka msafi kama ilivyokuwa Richmond. Atakacho enjoy hapo ni kukuangalia unavyohangaika baada ya kuona vyote ulivyomfanyia havijambadilisha. Binafsi nijitangaze kumfagilia Mheshimiwa Lowassa. Na ninamuombea usiku na mchana na ninajua (kwa Imani yangu) kuwa Mwenyenzi Mungu atasikia. Maombi yangu pamoja na ya Watu wote wenye mapenzi mema.
Mheshimiwa Lowassa, usirudi nyuma daima mbele... Na Mwenyenzi Mungu Akuwezeshe. Remember EYES ON THE PRIZE - We are with you ...all the way!

Anonymous said...

hakika Mh.EDWARD LOWASA NI TUNU,MM NAMPENDA KWAKUWA NI MTU AU KIONGOZI PEKEE AMBAYE KAVUMILIA MATUSI AMBAYO KATUKANWA NA WATOTO NDAN YA BUNGE NA PIA HATA WANACHAMA WAKE KUMUITA GAMBA LAKINI HAKUONESHA UDHAIFU WA KIUBINADAMU KUTUMIA POWER AU PESA YAKE KULIPIZA AU KUJIBU UBAYA ...
KINGINE KUWA NA POWER NA MAAMUZI MAZITO ..BINAFSI LOWASA HAKUNA WA KULINGANISHWA NAE JAPO NAE ANAMADHAIFU YAKE

Anonymous said...

unajua ukisoma kitabu cha daniel kwenye biblia ndio utajua alichofanyiwa lowasa. nasema tutaomba mchana na usiku mungu huyu tunayemtumkia ambaye amefanya mambo ya ajabu. huyu mungu atampaka mafuta lowasa. watasema sana lakini achana na mtu anayetembea na nguvu za mungu. ni hatari.

pia achana na mtu kama aliwahi kutenda dhambi na akatambua akatubu kwa mungu wake. fedha yake akarudisha fadhila kwa jamiii. huyo ni hatari ana mungu na mungu atampigania.tunamwombea usiku na mchana mpaka kieleweke. hatutatumia nguvu ila jina la mungu aliyehai. mungu ageuze mioyo ya watanzania na uwezo huo mungu anao. subirini mtanona kitakachotokea.

watu wanadai oooh lowasa anahonga. watu wanakosa fikra hivi mtu atoke kijiji kwenda wilayani kusaini fomu. bila nauli jamani. kuna kikao bila allowance? watanzania tuwe na akili yakupambanua mambo.

Post a Comment