Thursday, May 29, 2014

 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha moja ya tuzo za dhahabu ilizowahi kupata wakati wa mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.
 
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza ushindi wake wa tuzo la Ubora wa Kimataifa 2014 maarufu kama ‘International High Quality Trophy 2014’ katika mashindano ya Monde Selection. Safari Lager itapokea tuzo hiyo Jumatatu tarehe 2 Juni, mjini Bordeaux, Ufaransa.

Tuzo ya Ubora wa Kimataifa au ‘International High Quality Trophy’ ni tuzo ya heshima linalotolewa kwa bidhaa ambazo zinashinda tuzo za ‘Gold’ au ‘Grand Gold’ kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo. Safari Lager inepewa tuzo hiyo ya heshima kwa kuweza kushinda ‘Gold’ na ‘Grand Gold’kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo.

Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Bw. Oscar Shelukindo,  alisema, “Safari Lager ni bia ambayo siku zote nia yake ni kuridhisha wateja wake na kwa miaka yake yote…Tunaishukuru sana Monde Selection kwa heshima waliyotupa na hii inatupa motisha ya kuendelea kuwapa wateja wetu bia bora zaidi”.
 

0 comments:

Post a Comment