Wednesday, May 28, 2014


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi
BONDIA namba moja katika uzito wake wa  light welterweight ,  Ibrahimu Class 'King class Mawe' ameibuka na kukemea vikali tabia ya mabondia kwenda katika ngumi kuangali na kuona ni kama wanakwenda kwenye starehe 'picnic'

aliyazungumza hayo katika ukurasa wake wa facebook mapema hivi karibuni akipinga matukio yanayofanywa na mabondia wakubwa nchini tanzania kwa kuingia ukumbini uku wakiwa wanakunywa pombe wakiwa wameshika chupa mbilimbili

bondia huyo alienda mbali zaini kwa kuwaeleza kuwa bondia anapo kwenda kwenye ngumi yupo kazini kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine hivyo anapokwenda aijalishi anacheza au achezi kwa siku hiyo hivyo lazima uwe na nidhamu kwa mashabiki ili upate wapenzi wapya zaidi

mana wapenzi wa ngumi wanapatikana kwenye ngumi uwezi mpenzi anaekujua kukutambulisha kwa mwingine ohoo 'King Class Mawe' yule ameshika bia awezi kukubali hata siku moja sana sana atakwambia mbona bondia mwenyewe mlevi namna hile ile inapoteza mwelekeo wa mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini

Class aliongea hayo hivi karibuni baada ya mabondia Mada Maugo na Thomasi Mashali kuamua kuzipiga kavu kavu kwa kitu kilichotambulika kuwa wao ni walevi tena wakiwa katika ukumbi wa ngumi frends corner manzese

kitendo hiki cha kupigana ovyo sikiingi mkono hata siku moja wakati walishapigana uringoni sasa watafute promota ili wapigane tena

kitendo chao cha kupigana ovyo kinatukosesha thamani sisi mabondia chipkizi ambapo mchezo huu wa masumbwi tunautegemea na tunaupenda kwa kuwa tuna malengo nao

ushauli wangu kwa mabondia wasifanye kuwa kwenda kwenye ngumi wanaenda kwenye starehe na kama unajiona wewe mlevi bora ubaki nyumbani kwako unywe basi na si vinginevyo kwa kulewa mbele ya mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini tunaonekana mabondia wote walevi tafadhalini mabondia wenzangu na samahani kama nitakuwa nimekukwadha kwa habari hizi yote tufanye tushilikiane ili mchezo wa masumbwi usonge mbele

0 comments:

Post a Comment