Thursday, May 22, 2014


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara leo, Maei 21, 2014, kwenye Viwanja vya Stendi ya Ikungi, wilayani Ikungi mkoani Singida, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia za kuzitatua mkoani humo.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo wa Ikungi
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo wa CCM uliohutubiwa na Kinana kwenye Viwanja vya Stendi  Ikungi, Singida.
Mwananchi akiishangilia CCM baada ya kukabidhiwa kadi na Kinana kwenye mkutano huo
Aliyekuwa  Katibu wa tawi la Chadema, Ikungi, Ismail Gwau akitupa bendera ya chama hicho mbele ya Kinana na Nape baada ya yeye na wenzake kuamua kufunga tawi lote na kuhamia CCM wakati wa mkutano huo uliofanyika Stendi ya Ikungi.
Katibu huyo aliyekuwa wa Chadema akitupa pia kadi za chama hicho mbele ya Kinana wakati wa mkutano huo wa Ikungi
Gwau alionyesha kadi yake mpya ya CCM baada ya kupewa na Kinana kwenye mkutano huo
Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Makiungu, Ikungi, Mei 21, 2014
Nape akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Makiungu, Ikungi
Kinana akizungumza kwenye zahanati ya Kijiji, cha Kimbe, Ikungi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo ambao umekamilika lakini zahanati imeshingwa kuanza kutoa huduma kutokana na  nyumba  ya mganga kutokamilika kujengwa kutokana na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lisu na Diwani wake kudaiwa kuzuia wananchi kuchangia
Nape akiwa na mtoto Frank John (5) ambaye alimbeba alipomkuta wakati Kinana alipokagua zahanati hiyo,kwenye Kijiji cha Kimbe, Ikungi.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akishiriki kuvuna mazao kwenye shamba la Mjane Mayasa Mukhandi wa Kijiji cha Unyaghumpi Kata ya Mungaa, Ikungi, Kinana alipotembelea shamba hilo, leo, Mei 21, 2014.
Mjumbe wa Kamati Kuu, Khadija Aboud akishiriki kuvuna mazao kwenye shamba la Mjane huyo, Mayasa Mukhandi wa Kijiji cha Unyaghumpi Kata ya Mungaa, Ikungi
Nape akishiriki kuvuna mazao kwenye shamba la Mjane huyo, Mayasa Mukhandi wa Kijiji cha Unyaghumpi Kata ya Mungaa, Ikungi.
Kinana akimpatia Bi Mayasa Mukhando ambaye ni Mjane, fedha za kumsaidia kuvuna shamba lake,  katika Kijiji cha Unyaghumpi
Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya msingi ya Unyahongi, Ikungi Singida akiwa katika ziara hiyo leo, Mei 21, 2014.
Wananchi wakijitolea kwenye shule ya msingi Unyahongi, Ikungi
Mkurugenzi wa kampuni ya Singida Agriculture Ltd, Ali Mohamed, (kushoto) akimpa maelezo Kinana katika shamba la kampuni hiyo la kilimo cha Umwagiliaji kwa matone, eneo la Mkiwa, Ikungi
Mkurugenzi wa kampuni ya Singida Agriculture Ltd, Ali Mohamed,akimpa maelezo Kinana eneo la Mkiwa, Ikungi
Msafara wa Kinana wakitazama bwawa la mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa matone kinachoendeshwa na kampuni ya Singida Agriculture Ltd, eneo la Mkiwa, Ikungi
Nape akijaribu kulima kwa trekta kwenye shamba la kampuni hiyo
Kinana akipatiwa maelezo na mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Kilimo kuhusu wanavyohifadhi mazao kwenye makasha kabla ya kusafirisha.
Nape akisaidia kupanga kwenye vifaa maalum maharage yanayolimwa kwenye mashamba ya kampuni hiyo ya kilimo. Picha zote na Bashir Nkoromo, theNkoromo Blog

MBARONI KWA KUMFICHA MTOTO KATIKA BOX MIAKA 4

 Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni  baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box  kwa miaka  4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
 Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.

Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa. Habari zaidi soma hapo chini.

 MUME na mke  wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa  tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
 
Kamanda  wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20  mwaka huu majira ya saa 4.45  Asubuhi  katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
 
Alisema majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
 
Alimtaja mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi  mine na nusu  ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili kuendela nayo.
 
Afisa Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na afya dhoofu.
 
Alisema alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said  na Mume wake Mtonga Omari.
 
 
 Baba mzazi wa mtoto huyo alisema  yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
 
Alisema kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
 
 
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema  akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
 
Zongo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi  kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
 
Zongo  alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
 
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji)  kutoa taarifa polisi.
 
 
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo  alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
 
 
Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
 
   Hores Isaack Msaky  Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa matibabu ya awali .
 
‘’ Tulimfanyia   vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
 
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
 
Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke  kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.
 
Baadi ya mashuhuda wa tukio  hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita na kwamba  Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
 
 Hata hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina  kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.

0 comments:

Post a Comment