Saturday, May 17, 2014Seleman

 Dar es Salaam,
Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini, Suleiman Galile ”tall” anategemea kupanda tena ulingoni Mei 24 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam, kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika pambano lisilo la ubingwa la uzito wa kg76.
Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo, Katibu wa ngumi za kulipwa nchini, ambaye ndiye anayesimamia mapambano yote ya utangulizi, Bw. Ibrahim Abbas Kamwe alisema, Galile na Dula wamekubaliana kusheza siku hiyo ya Jumamosi ya Mei 24, huku wakisindikizwa  na Karama Nyilawila na Said Mbelwa.
Watakaogombania ubingwa wa UBO,hapo awali ilipangwa Karama kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari.
Pia siku hiyo kutakuwepo na  mapambano mengi ya utangulizi yenye ushindani , wakati  Adam Ngange akimkabili Alan kamote wa Tanga, zumba kukwe atazipiga na kamanda wa makamanda,Seleman Zugo na Manyenza,  Ramadhan Kumbele ataoneshana umwamba na Hassan Kiwale “Moro best”, wakati Bakari Dunda atapambana na Mbena Rajabu.
Madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi, Idd Athuman atacheza na Julias Thomas Kisarawe, wakati Mwaite Juma atachuana na Daudi Giligili.
 Kamwe alimaliza kwa kusema mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli .

0 comments:

Post a Comment