Tuesday, May 6, 2014

 
Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Wa pili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akishangilia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi(kushoto).
 
Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Kulia ni Betrice Madafu kutoka chuo hicho akwa ameshikilia kitita cha fedha taslimu Shilingi 2,500,000/=,Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akishangilia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi.
 
Afisa Tarafa wa Moshi mjini, William Issa(kushoto) akimkabidhi  Nahodha wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa, Said Mohamed kitita cha fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zlizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.Kulia ni Betrice Madafu kutoka chuo hicho na katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

Wachezaji wa timu ya Chuo cha RUCCO cha Iringa wakishangilia na kikombe  pamoja na fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za “Safari Higher Learning Pool Competition 2014” zilizomalizika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.RUCCO waliupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John 13-12
 
Na Mwandishi Wetu.Moshi
CHUO cha RUCCO cha mkoani Iringa kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa yaliyoyoshirikisha mabingwa wa Vyuo vya Elimu ya juu kutoka mkoa minane yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Aventure Moshi -Kilimanjaro.
RUCCO ilifanikiwa kupata ubingwa huo kwa kukifunga chuo cha St. John cha Dodoma 13-12, na hivyo kuzawadiwa kikombe na  fedha taslimu Shilingi 2,500,000/= .
Nafasi ya pili ilichukuliwa na St. John ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha Ardhi cha Dar es Salaam kwa kukifunga chuo cha Muccobs 13-8 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,300,000/= na nafasi ya nne ikaenda kwa wenyeji wa mashindano hayo Muccobs ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,000,000/=.
Timu zingine ambazo hazikufanikiwa kufikia hatua ya nne bora zilizawadiwa kifuta jasho cha fedha taslimu shilingi 500,000/= kwa kila chuo ambavyo ni chuo cha TIA,Bugando,Sua na Mzumbe.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Fredrich Mwangata kutoka chuo cha SAUT Mwanza alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Taifa na kuzawadiwa Ngao pamoja na fedha taslimu  Shilingi  300,000/=  kwa kumfunga Steven Kyasi kutoka Chuo cha Mzumbe Mbeya 4-0,ambaye alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=
Nafasi ya tatu ilichukuliwa Justus Mhando kutoka chuo cha Mipango Dodoma ambaye alizawadiwa Shilingi 150,000/= na nafasi ya nne alichukua  Ally Jamson wa Muccobs Moshi na kuzawadiwa 100,000/=.
Upande wa kinadada Jacline Molel kutoka chuo cha TIA alitwaa ubingwa wa Taifa na kuzawadiwa ngao pamoja na fedha taslimu Shilingi 200,000/= kwa kumfunga Deborah Ramadhani  kutoka chuo cha SILA Arusha 3-0 na hivyo Debora kushika nafasi ya pili na kuzawadiwa Shilingi 150,000/=. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rehema Uzi kutoka Chuo cha UDOM ambaye alizawadiwa Shilingi 100,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na Beatrice Madafu kutoka RUCCO ambaye alizawadiwa Shilingi 50,000/=
Fainali za Kitaifa zilishilikisha mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoa wa Kilimanjaro.
 

 
 

0 comments:

Post a Comment