Thursday, May 22, 2014


 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba, akizungumza jambo katika kikao cha wadau wa muziki juu ya ujio wa mwili wa marehemu Amina Ngaluma, anayeletwa kesho usiku ukitokea nchini Thailand, alipofia. Anayefuata ni mume wa marehemu, Rashid Sumuni, Mwinjuma Muumini na Said Mdoe aliyeshika kidevu. 
Katika kikao hicho, Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere alionyesha kuchukizwa vikali na ujio mdogo wa wadau wa muziki kujadili kuletwa kwa marehemu. Steve aliwataka waimbaji na wasanii wote kuwa makini pamoja na kushirikiana wao kwa wao ili wajiwekee mazingira mazuri. 
Katika kikao hicho, ilitangazwa kuwa jumla ya shilingi milioni tano zinahitajika kufanikisha mazishi ya mkali huyo nchini, akikumbukwa sana na wimbo wake Mgumba namba 2, akiwa ndani ya Double M Sound, chini ya Mwinjuma Muumini.
 Rais wa Bongo Movie Tanzania, Steve Nyerere akichangia hoja katika kikao hicho cha kujadili msiba huo, ambapo jumla ya shilingi milioni tano zinahitajika ili kuhakikisha kuwa mwili wa Amina unawasili na kuzikwa kama inavyostahiki.
Miongoni mwa wadau waliojitokeza katika kikao hicho wakisikiliza kwa umakini juu ya kikao cha wadau wa muziki wa dansi juu ya msiba wa Amina Ngaluma. Kikao hicho kilifanyika leo saa tano asubuhi katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment