Tuesday, May 13, 2014

 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya pili ya washindi sita wa kila wiki wa kampeni ya bia ya Castle Lager ijulikanayo kwa “Castle Lager Perfect 6” iliyochezeshwa Dar es Salaam leo.Kushoto ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Humudi Abdulhussein na mratibu wa kampeni hiyo, Lawrence Andrew.

Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Bia nchini Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager leo wametangaza washindi 6 wa droo ya pili  katika kampeni ya castle lager iliyochezesha jijini Dar es Salaam kwa wateja wa bia hiyo ijulikanayo kama “Castle Lager Perfect 6” ambapo wateja wote 6 wamejishindia fedha taslimu Shilingi 100,000/= kila mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo alisema kampeni hii itakwenda kwa muda wa wiki 10 na kila wiki wateja kumi watazawadiwa kama tulivyofanya leo hii.
Alisema Kabula baada ya kumaliza droo zote washiliki wote wataingia kwenye droo kubwa na washindi wawili wataambatana na timu ya watu sita watakaoibuka mabingwa katika bonanza  zitakazoshirikisha timu za bar mbalimbali, ambapo mabingwa hao (6) wataungana na washindi wawili kushuhudia mechi ya Barcelona Spain pamoja na kuangalia sehemu mbalimbali za historia za timu hiyo.
Gharama za usafiri pamoja na malazi zote zitagharamiwa na TBL, kupitia bia yake ya Castle Lager alisema Fimbo Butallah.
Washindi waliopatikana mwaka huu ni Rexavel Ronard (46) mkazi wa Karakata Dar es Salaam, John Albogast (49) mkazi wa Sinza Dar es Salaam, Steven Mbaga (30) Mabibo Dar es Salaam, Harrid Jaffary (35) Kigamboni Dar es Salaam, Evarist Kilimo (53) mkazi wa Morogoro na wa mwisho hakutaja jina lake mwenye namba ya simu 0712 207594.
Katika kampeni hii wachezaji wa mpira ambao nio wazoefu kwa maana ya kwamba wachezaji wa Ligi Kuu hawaruhusiwi kushiriki kampeni hii,ni kwa wateja wa castle Lager tu na ambao hawachezi Ligi Kuuu alisema Kabula.
Namna ya  kushiriki ni unanunua bia ya Castle Lager,kwenye mfuniko kuna namba,tuma meseji kwenye namba hiyo utakuwa umeshiriki  kwenye droo ya kila mwezi ila vigezo na masheriti vinazingatiwa kwani hawaruhusiwi kushiriki chini ya umri wa miaka 18.
Kampeni hii ilianzia jijini Dar es Salaam na sasa iko njiani kuelekea jijini Mwanza,Morogoro, Arusha pamoja na mikoa mingine.

0 comments:

Post a Comment