Wednesday, June 4, 2014

 
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini wa mashindano ya ngoma yajulikanayo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” TBL Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja matukio wa Taifa TBL, George Mombeki.

Meneja matukio wa Taifa TBL, George Mombeki(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini wa mashindano ya ngoma yajulikanayo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” TBL Dar es Salaam.
 
  BIA ya Balimi Extra Lager imefurahi kutangaza udhamini wake wa Mashindano ya Ngoma za Asili kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. Mashindano haya yanatarajiwa kuanza Jumamosi Tarehe 7 Juni 2014 na itashirikisha mikoa 6. 

Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania. Mikoa 6 itakayoshiriki katika mashindano haya ni: Tabora, Shinyanga, Bukoba, Kahama, Mwanza na Musoma. 

Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa katika mkutano na waandishi wa habari alisema, “Utamaduni ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu, ni lazima tuenzi na tuzikumbuke. Ni hali ya kusikitisha pale ambapo watu hawajui tamaduni zao kwani utamaduni unaweza kutueleza mambo mengi kuhusu vitu ambazo tunanya sasa”. 

Finali za kila mkoa zinatarajiwa kuwa kama ifwatavyo:

1.    Mkoa wa Tabora; Jumamosi tarehe 7Juni 2014           

2.    Mkoa wa Shinyanga; Jumamosi tarehe 14 Juni2014   

3.    Mkoa wa Bukoba; Jumamosi tarehe 21 Juni 2014       

4.    Mkoa wa Kahama; Jumamosi tarehe 27 Julai 2014                 

5.    Mkoa wa Mwanza; Jumamosi tarehe 2 Agosti 2014

6.    Mkoa wa Musoma; Jumamosi tarehe 9 Agosti 2014                

7.    Mashindano ya Kanda; Jumamosi tarehe 16 Agosti 2014    

Zawadi za kushindania ni: 

ZAWADI
NGAZI YA MKOA
NGAZI YA KANDA
Mshindi wa Kwanza
600,000
1,100,000
Mshindi wa Pili
500,000
850,000
Mshindi wa Tatu
400,000
600,000
Mshindi wa Nne
300,000
500,000
Mshindi wa Tano hadi wa Kumi kila kikundi
150,000
250,000

0 comments:

Post a Comment