Tuesday, June 10, 2014

 
Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Ndovu High International Quality Trophy) iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.Nyuma ni Mpishi wa bia wa Kampuni ya bia nchini(TBL), Cavin Nkya.


Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Safari Lager High International Quality Trophy iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
 
Picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Ndovu High International Quality Trophy) iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
  KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia zake za Safari Lager  na Ndovu Special Malt leo zimewasili nchini zikiwa na tuzo za ubora wa kimataifa 2014 maarufu kama ‘International High Quality Trophy 2014’ katika mashindano ya Monde Selection yaliyofanyika Bordeaux  nchini Ufaransa.

Tuzo ya Ubora wa Kimataifa au ‘International High Quality Trophy’ ni tuzo ya heshima inayotolewa kwa bidhaa ambazo zinashinda tuzo za ‘Gold’ au ‘Grand Gold’ kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo. Ndovu Special Malt na Safari Lager  zimepewa tuzo hizo za heshima kwa kuweza kushinda ‘Gold’ na ‘Grand Gold’kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema, “Ni heshima kubwa sana kwetu kutambuliwa katika ngazi za kimataifa. Tuzo hii inatupa motisha wa kuzidi kuimarisha ubora wa Ndovu Special Malt, kuongeza ubora ili kuwaburudisha wateja wetu zaidi”.

“Tunafurahi sana kuweza kuipa bia ya Kitanzania umaarufu duniani kutokana na ubora wake. Tungependa kuishukuru Monde Selection kwa kuanda shindano hili ambalo linatambua na kuzawadia kilicho bora. Tuzo hii sio tu kwa TBL Ndovu Special Malt, bali ni kwa Tanzania nzima” alisema Bi. Pamela Kikuli.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Bw. Oscar Shelukindo,  alisema, “Safari Lager ni bia ambayo siku zote nia yake ni kuridhisha wateja wake na kwa miaka yake yote…Tunaishukuru sana Monde Selection kwa heshima waliyotupa na hii inatupa motisha wa kuendelea kuwapa wateja wetu bia bora zaidi”.
Shelukindo alimaliza kwa  kutoa wito kwa wateja wa Safari Lager kuendelea kutumia bia hiyo kwani ndio bia namba moja kwa ubora na kwa mauzo Tanzania na pia ni bia namba moja Afrika na leo hii tunapozungumza imepata heshima ya pekee ya ubora wa kimataifa.
Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah alimaliza kwa kuwashukuru kwanza wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuzifanya bia ya Safari Lager na Nduvu Special Malt kupata tuzo hizo, lakini pia aliwashukuru watanzania wote wanaoendelea kuzisapoti bia hizo mpaka leo hii zinaendelea kuwa bia bora kimataifa  ambapo pia alitoa wito kwa watanzania kuendelea kunywa bia ya Safari na Ndovu pamoja na bia zingine zinazotengenezwa na Kampuni ya bia Tanzania(TBL) ili ziendelee kupata heshima ya pekee kimataifa.

 
Picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitoka Ufaransa kuchukua tuzo ya Ubora wa Kimataifa(Safari Lager High International Quality Trophy) iliyoshinda hivi karibuni kutoka katika taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa.
 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli (kulia) akimkabidhi Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam, Calvin Martin tuzo iliyopata bia ya Ndovu Special Malt mara baada ya kuwasili kutoka nchini Ufaransa(Ndovu High International Quality Trophy) Dar es Salaam
 
Mpishi wa bia wa Kampuni ya bia nchini(TBL), Cavin Nkya(katikati) akimkabidhi Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam, Calvin Martin tuzo iliyopata bia ya Safari Lager mara baada ya kuwasili kutoka nchini Ufaransa(Safari Lager High International Quality Trophy) Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
 Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (katikati) akimkabidhi Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Dar es Salaam, Calvin Martin Medalo ya dhahabu iliyopata bia ya Safari Lager mara baada ya kuwasili kutoka nchini Ufaransa(Safarai Lager High International Quality Trophy) Dar es Salaam
 
Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akigonga chiazi na baadhi ya wafanyakazi wa Kapuni ya bia nchini(TBL) wakati wa hafla ya kujipongeza kwa kupata tuzo za ubora wa kimataifa kwa  Ndovu Special Malt  na Safari Lager Dar es Salaam jana.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakijipongeza kwa kushinda tuzo mbili kwa pamoja.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakijipongeza kwa kucheza muziki mara baada ya kushinda tuzo mbili kwa pamoja.

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakijipongeza kwa kucheza muziki mara baada ya kushinda tuzo mbili kwa pamoja.

0 comments:

Post a Comment