Wednesday, June 11, 2014
 
 KING CLASS- MAWE

                               -----------------------------

Kwa moyo mkunjuifu wenye furaha na bashasha tele organaizesheni yetu ya ngumi za kulipwa tanzania [TPBO LTD] Tunampongeza sana bondia chipukuzi wa ngumi za kulipwa tanzania IBRAHIMU CLASS,Kwa kushinda pambano lake la kugombea ubingwa wa SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA LA DUNIA [WPBF-]wa bara la afrika.

bondia ibrahimu class mwenye rekodi ya mapambano 11 na kushinda mapambano 10 na kushindwa moja jumamosi ya tarehe 08-06-2014 alimshinda bondia mzambia mwasa kabinga  katika pambano lilofanyika katika uwamja wa mpira wa ARTHUR DAVIS STADIUM ulioko zambia.

class alishinda pambano hilo ka TKO ya rundi ya 9 na kuwa bingwa wa kwanza kuuleta rasmi ubingwa wa WPBF -USBA kwa mara ya kwanza tangu shirikisho hilo lianzishe uhusiano wa kimichezo na tanzania.


WPBF- lenye makao yake makuu nchini marekani hapa nchini tanzania  inawakilishwa na MH  yassin abdallah [ustaadh] ambaye pia ni rais wa TPBO-LIMITED ,na vilevile akishikilia wadhifa wa makamu wa pili wa rais wa SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI [E&CAPBF].

Kwa kweli Tumefarijika sana kuona bondia chipukizi kama IBRAHIM CLASS anawakilisha taifa la tanzania katika masumbwi ya kulipwa na kuibuka bingwa akiwa ugenini ,jambo ambalo mabondia wakonge wanapoteza mapambano yao ya ugenini pamoja na kuwa na majina makubwa yanayowika nchini.
lengo la TPBO-LTD ni kuona dhamira yetu ya kuukuza mchezo wa ngumi za kulipwa ambao pia ni ajira ,kwa kuwekeza kwa mabondia chipukizi.

tanzania tunao mabondia chipukizi wengi na wenye uwezo mkubwa sana wakiwemo FRANCIS MIYEYUSHO,JUMAFUNDI,RAMADHANI
SHAURI,NASIBU RAMADHANI,MWAITE JUMA ,FRED SAYUNI, MOHAMED MATUMLA na wengineo wengi ambao kama wakipata msaada wa kudhaminiwa na kupatiwa michezo mingi ,ni imani yangu kwamba tutawapata akina rashid matumla wapya wa ukweli ambao wataitangaza vyema nchi yeyu TANZANIA.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa bondia IBRAHIMU CLASS kuzipiga nje ya nchi ya tanzania na amefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa WPBF- afrika.ni jambo la faraja sana kwa mustakbari wa ngumi za kulipwa nchini tanzania.
TPBO-LIMITED inalipongeza sana jopo la makocha ambao ndiyo wamemsaidia sana IBAHIM CLASS kuutwaa ubingwa huo,wakiongozwa na KOCHA MKONGWE MZEE HABIBU KINYOGOLI,KONDO NASSOR,SUPERD COACH ,NA SAKWE MTULYA kwa kazi nzuri sana waliyoifanya.

TPBO-LIMITED inaahidi kumsaidia bondia CLASS kwa kumtafutia mapromota wa uhakika ambao watamuandalia mapambano ya kutetea ubingwa wake huo mara kwa mara ili asiupoteze ubingwa wake kwa kushindwa kuutetea.

pia ninamuonya CLASS asilewe sifa kwani wako mabondia hapa nchini wamepoteza muelekeo na kupoteza uwezo wa mchezo kwa kushuka viwango sababu ya kulewa sifa baada ya kupata umaarufu.

                                 IMEANDIKWA NA KULETWA KWENU NAMI ;-

                               yassin abdallah mwaipaya- ustaadh
                              ------------------------------

-------
                                        RAIS- TPBO-LTD
                            mwakilishi wa WPBF-nchini tanzania

                               ,makamuu wa kwanza wa rais ;-
            SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI [E&CAPBF]

0 comments:

Post a Comment