Wednesday, June 11, 2014

Meneja wa  Mauzo wa TBL Robert Kaziwa akikabidhi  zawadi ya kitita cha shilingi laki Sita kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za Asili mkoa wa Tabora ambao ni Magereza Arts Group.
Mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Ugobhogobho ngoma ya asili ya jamii ya kabila la Wasukuma ambao walijinyakulia kiasi cha shilingi laki tano kati ya washiriki wa vikundi tisa vya ngoma mashindano ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya bia nchini TBL chini ya udhamini wa bia yake ya Balimi.
Kikundi cha JKT Tabora kiliibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mnadani Tabora mjini.
Kikundi cha Magereza wakati wa michuano hiyo
Kundi la Ugobhogobho wakati likionesha mambo yake
Kikundi cha hiari ya Moyo ambacho kilishika nafasi ya Saba na kujinyakulia shilingi Laki moja na nusu.
Kundi la ngoma ya asili lijulikanlo kama Wembe ambalo lilishika nafasi ya nane katika mashindano hayo.
Kundi la ngoma ya asili linalojulikana kama Uvikuja ambalo lilishika nafasi ya tano.
Baada ya kuibuka na ushindi huo kundi la Magereza lilianza kushangilia kwa mbwembwe za aina yake huku umati mkubwa wa wadau wa ngoma za asili wakishuhudia tukio hilo
 

0 comments:

Post a Comment