Wednesday, June 4, 2014


DSC_0340
Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP) Simon Sirro akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa makamanda wa Jeshi hilo nchini, mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP yana lengo la kuwajengea uwezo makamanda jinsi ya kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii. Kushoto ni Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan na kulia ni wakufunzi kutoka Uingereza, Adrian Barnes (kulia) na Alan Binks (wa pili kulia).
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
JESHI LA POLISI nchini limejisifu kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi yao kwa kuruhusu maandamano mengi kufanyika hapa nchini na ni maandamano machache tu yaliyowahi kupigwa marufuku. MOblog inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa maofisa 88 wa Jeshi la Polisi yanayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (UNDP) kupitia mradi wa Uwezeshaji Demokrasia (DEP), Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro amesema mafunzo hayo kwa makamanda ni kusaidia uelewa wao katika kupambana na maandamano au dalili za uvunjifu wa amani bila kuleta madhara makubwa kwa jamii.
“mafunzo haya kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini litasaidia kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu na utawala bora ili kudumisha amani na utulivu nyakati za uchaguzi,” amesema Sirro.
DSC_0310
Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP, William Hogan akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mafunzo hayo na muhimu wake katika kudumisha amani na kusaidia uchaguzi kufanyika katika hali ya utulivu na kidemokrasia zaidi.
Kamanda Sirro amesema kwamba mafunzo hayo yanalenga pia kusaidia uelewa makamanda jinsi ya kushughulika na wavunjifu wa amani kwa kuzingati weledi wa Jeshi la Polisi nchini.
Amesema kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani 2015 mafunzo yamekuja wakati mwafaka kwa Jeshi la Polisi kupanua wigo wao katika maswala haya ya utawala bora na haki za binadamu nchini.
“utafiti unaonyesha kwamba maandamano mengi yamewahi kuruhusiwa na Jeshi la Polisi kuzidi yale yaliyopigwa marufuku kwa hiyo yana ya kwamba jeshi linazuia haki za raia kukusanyika au kuandamana haipo isipokuwa kwa sababu za kiusalama tu,’ aliongeza Kamanda Sirro
Kwa upande wake, Mtaalamu wa Uchaguzi, kutoka UNDP, William Hogan amesema kuwa mafunzo hayo yanahusu kumudu kuleta utulivu wa umma na yanaendeshwa katika ukumbi wa maofisa wa Polisi wa Oysterbay na ukumbi wa maofisa w Polisi Zanzibar.
DSC_0316
DSC_0325
Baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha kutuliza ghasia nchini (FFU) nchini wakifuatilia hotuba za Kamanda Sirro wakati ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo wa makamanda wa polisi wa kupanga, kumudu na kuratibu kwa ufanisi hatua za kipolisi za kushughulikia matukio yanayotishia utulivu katika jamii.
“kupitia program hii ya mfululizo wa kozi nne zitakazodumu kwa majuma mawili kila moja, maofisa 88 ngazi za kati na juu kutoka kila mkoa katika nchini watafunzwa na wakufunzi waandamizi nane kutoka katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi cha Uingereza,” amesema Hogan
DSC_0317
DSC_0361
Mgeni Rasmi Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini (SACP), Simon Sirro aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
DSC_0355
SACP Simon Sirro akiteta jambo na Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka, UNDP, William Hogan baada ya picha ya pamoj

0 comments:

Post a Comment