Tuesday, June 24, 2014

 
Nahodha wa Klabu ya Billiard,Becka Mbulla (katikati) akihesabu  fedha taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Pool Mkoa wa Mwanza yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
 
Nahodha wa Klabu ya Billiard,Becka Mbulla (kulia) akitoa fedha taslimu Shilingi 800,000/= kwenye bahasha mara baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Bernard Issaria(kushoto) mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Pool Mkoa wa Mwanza yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.Katikati ni Katibu wa chama cha Pool Mkoani humo, Switbart Victor.

Na Mwandishi Wetu.

KLABU ya Billiard ya Mwanza,New Stand ya Shinyanga na Yakwetu Pwani  zimefanikiwa  kutwaa ubingwa  wa mikoa katika fainali za mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya Mikoa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mikoani humo na kuzawadiwa kila klabu ferdha taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa  kwenye fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Billiard ya Mwanza ailitwaa ubingwa kwa kuifunga Klabu ya Wanyama 13-11, New Stand ya Shinyanga ilitwaa ubingwa kwakuifunga klabu ya The Ganner 13-7 na Yakwetu ya Mkoa wa Pwani ilitwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya Kiluvya 13-12.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Mwanza,Lameck Omary(Ndala Ndefu) alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/=  kwa kumfunga Hans Fabian 5-2 ambapo Hans Fabian alizawadiwa fedha taslimu Shilingi  250,000/=.Mkoani Shinyanga,Paul Filaki  alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/=  kwa kumfunga Fredrick Njele3-0 ambapo Fredrick Njele alizawadiwa fedha taslimu Shilingi  250,000/=.na Mkoa wa Pwani, Anold Djofu alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/=  kwa kumfunga Michael Njau 3-2 na hivyo Michael Njau alizawadiwa fedha taslimu Shilingi  250,000/=.

Mchezaji mmoja mmoja Wanawake waliofanikiwa kutwaa ubingwa ni, Mwanza- Rukia Issa,Shinyanga-Sada Tullah na Pwani ni Fatma Kihongo ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= kila mmoja  pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.

0 comments:

Post a Comment