Tuesday, June 3, 2014


Meneja Mauzo Unilever Tanzania wa eneo la Mbeya Rajab Kondo (kushoto) akimkabidhi mshindi wa promosheni ya 'Fua Upae', Marcko  j. Fihavango fedha taslimu sh. 600,000 baada ya kununua sabuni ya Omo. Katikati ni Balozi wa Omo Tanzania, Mariamu Migomba.Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika Beaco Hotel  jijini Mbeya  jana.Meneja uhusiano wa kampuni ya unilever Tanzania  Nicholaus John ametoa wito kwa wananchi na wateja wote wa mkoa wa Mbeya  kuichangamkia fursa hiyo ya kipekee na kuongeza kuwa zoezi hilo na promosheni hiyo ni la ukweli hivyo hawanabudi kuipokea kwa moyo wote kwani bado zawadi nyingi zitaendelea kutolewa kwa washindi huku kampuni hiyo ikijipanga zaidi kwa siku za baadaye kuja na promosheni nyingine tofauti tofauti zenye lengo la kurejesha shukurani kwa wateja.

Balozi wa Omo Tanzania, Mariamu akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani


Picha ya pamoja

0 comments:

Post a Comment