Wednesday, August 27, 2014

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Mwanza, Christopher Fuime(kulia) akimkabidhi kikombe kiongozi wa kikundi cha ngoma cha Bujora mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza .
Baadhi ya wacheza ngoma wa kikundi cha Bujora wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu shilingi 1,100,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza.
Bujora mabingwa Balimi Ngoma Kanda ya Ziwa 2014.
Na Mwandishi Wetu.
KIKUNDI cha Ngoma za asili cha Bujora cha jijini Mwanza kimefanikiwa kuchukua ubingwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili kanda ya ziwa mwishoni mwa wiki  kwa pointi 87.5 zilizofanyika katika Uwanja wa Mabatini  kwa kushirikisha mabingwa wawili kutoa katika mikoa mitano ambayo ni Tabora, Shinyanga, Kagera,Mara na Mwanza.
Kwa ubingwa huo kikundi cha Bujora kilizawadiwa pesa taslimu shilingi 1,100,000/= , kikombe pamoja na medali za dhahabui cha Mwanalyaku ambao walipata pointi .
 Nafasi ya Pili katika fainali hizo ilichukuliwa na kikund Mwanalyaku cha jijini Mwanza pia kwa pointi 79.5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi  850,000/=
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Bugoloile cha Kagera kwa pointi 79.3 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=.Nafasi ya nne ilikwenda kwa kikundi cha Mabulo ya Jeshi cha Sinyanga kwa pointi 76.7 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=.
Nafasi ya tano mpaka ya kumi ni kikundi cha Rugu kagera pointi 75.2,Musoma One cha Mara 73.8,Wanunguli Shinyanga pointi 73.1,Magereza Tabora 70.1,Kiwajaki Mara 69.6 na cha mwisho ni kikundi cha Bugobogobo cha Tabora pointi 59.3.
Mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime ambaye aliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuzamini mashindano ya ngoma ambayo hufanyika kila mwaka wakati wa mavuno ambapo aliwaomba waendelee kudhamini kwani yanatukumbusha asili yetu tulikotoka na pia zawadi wanazopata zinaongeza kipatao kwa washiriki.
Nae Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edithi Bebwa aliwashukuru washiriki wote kwa kuwa mabingwa wa mkoa yao huko wanakotoka na pia aliwashukuru kwa kushiriki fainali za Kanda na kuwaahidi kuboresha zaidi mashindano mwaka ujao hasa upande wa zawadi.
Edithi alisema sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).                              

  

0 comments:

Post a Comment