Friday, September 19, 2014

 Mabingwa wa mchezo wa Safari Pool 2014, Klabu ya Topland ya Mkoa wa Kimichezo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakipokelewa kwa shangwe na mashabiki mara baada ya kuwasili klabuni kwao Magomeni wakitokea mkoani Kilimanjaro. 
 Mabingwa wa mchezo wa Safari Pool wa Klabu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Dar es Salaam wakishangilia kwa kucheza mara baada ya kuwasili klabuni kwao  Magomeni wakitokea Mkoani Kilimanjaro. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Pool wa Mkoa wa kimichezo Kinondoni(KIPA), Goodluck Mmari (kulia) akimkabidhi mkurugenzi wa klabu ya Topland,Fredrick Kiando kikombe mara baada ya timu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Pool Taifa 2014 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Kilimanjaro. 


0 comments:

Post a Comment