Wednesday, September 3, 2014

 Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi kikombe nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo ujulikanao kama “Safari National Pool Competition 2014”  ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu.
 Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi 800,000/= nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu.

 Baadhi ya wachezaji wa Pool wa klabu ya Mpo Afrika na mashabiki wakishangilia na kikombe mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wa klabu ya Delux na mashabiki wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”, mkoa wa kimichezo wa Temeke jijini Dar es Saalaam na Dodoma zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa mwishoni mwa wiki.
Mkoa wa kimichezo wa Temeke mabingwa ni klabu ya Mpo Afrika walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa mwaka jana wakati mkoani Dodoma Klabu ya Delux ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo.
Klabu ya Mpo Afrika na Delux kwa kutwaa ubingwa huo zilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= kila klabu pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Temeke; Innocent Sammy alifanikiwa kutwaa ubingwa na Dodoma ni Regnald Kassimu,  ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja mmoja Wanaume.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake,Temeke; Rebeca Magaigwa alitwaa ubingwa na Dodoma ni Rehema Mussa, ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja mmoja upande wa Wanawake.
Wiki hii fainali za Safari Pool Competition 2014,ngazi ya mikoa zinatarajiwa kuhitimishwa  na mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya.
Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.


0 comments:

Post a Comment