Friday, September 19, 2014


 Nahodha wa timu Topland ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Patrick Nyangusi akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Topland wa mkoa wa kimichezo wa Kinondoni wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu Shilingi 5,000 000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Topland wa mkoa wa kimichezo wa Kinondoni wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu Shilingi 5,000 000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.Nnyma ni Menyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kinondoni, Goodluck Mmali(Meeda)

Na Mwandishi Wetu.Moshi
KLABU ya Topland ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni yenye makazi Magomeni jijini Dar es Slaaam imefanikiwa kutetea ubingwa wa ke wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro kwa kuifunga timu ya Anatory ya Mkoani Morogoro 13-3.
Timu ya Topland kwa kutwaa ubingwa huo ilizawadiwa Kikombe,Medali za dhahabu na pesa taslimu Shilingi 5,000 000/= wakati mshindi wa pili Anatory ya Morogoro walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,500 000/= pamoja na medali za fedha.
Mshindi wa tatu katika fainali hizo ni timu ya Mashujaa kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala jijini Dar es Salaam ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,250,000/= pamoja na medali za shaba wakati washindi wanne ni timu ya Mboya ya Mkoani Kilimanjaro ambao ndio walikuwa wenyeji wa Mashindano hayo kwa mwaka 2014 ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi  750,000/=.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Mussa Mkwega kutoka klabu ya Anatory ya Mkoani Morogoro alitwaa ubingwa kwa kumfunga Innocent Sammy kutoka Mkoa wa kimichezo wa Temeke 5-4 na hivyo Mkwega kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=,medali ya dhahabu pamoja na ngao wakati Innocent Sammy kwa kuchukua nafasi ya pili alizawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na medali ya fedha.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wakina Dada, Neema Hamis kutoka Mmkoa wa Tanga alitwaa ubingwa kwa kumfunga  Sada Tulla kutoka Shinyanga na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 350,000/= pamoja na medali ya Dhahabu wakati  Sada Tullah yeye kwa kukamata nafasi ya pili alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 200,000/=
Akikabidhi zawadi hizo Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya afari Lager kwa kudhamini mashindano ya Pool Taifa na alliwaomba waendelee kufadhili kwani mpaka sasa ni mchezo pekee ulioiletea sifa Nchi kupia fainali za Afrika ambapo Mtanzania Patrick Nyangusi anashikilia Ubingwa wa Afrika.
Nkamia aliwataka pia Chama cha Pool Taifa(TAPA) kutumia vyema fursa ya TBL kwa manufaa ya kuendeleza mchezo huo nchini na Kimataifa na kwa jinsi hiyo aliwapa siku 60 wawe wameshafanya uchaguzi na kupata viongozi wa kuchaguliwa kikatiba na wa muda tangu chama hicho kianzishwa kama ilivyo sasa.
Mwisho Waziri Nkamia aliwatakia safari njema wanamichezo wote kurejea majumbani salama na  kuwaomba walichokipata kwa Safari Lager kama zawadi wakakitumie vyema kwa maezndeleo yao. 
          

0 comments:

Post a Comment