Sunday, October 19, 2014
Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (kulia), akiondosha mpira wa hatari katika eneo la langoni kwake huku mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri (katikati) akijaribu kunyoosha guu ili kupiga mpira huo bila mafanikio wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomaliziki jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bila timu hizo kufungana. Kushoto ni Kelvin Yondan, akijiandaa kutoa msaada.

MATOKEO KAMILI YA MECHI ZA LIGI KUU KATIKA VIWANJA SITA HII LEO:-

YANGA 0- SIMBA 0
NDANDA FC 1- RUVU SHOOTING 3
Wafungaji Ndanda ni Salim Mineli dk 80
Wafungaji Ruvu Shooting ni Juma Nade dk 10, Abdallah Mussa dk 48, Mathew Willson dk 75.

POLISI MORO 0- MTIBWA SUGAR 0
COASTAL UNION 2- MGAMBO JKT 0
Wafungaji Coastal ni Rama Salim dk 29 kwa penati na Keneth Masumbuko dk 89.

MBEYA CITY 0- AZAM FC 1
Mfungaji ni Agrey Morris 
Kipa wa Yanga Deogratias Munishi akiruka kudaka mpira wa krosi mbele ya mshambuliaji wa Simba Elius Maguri.
Mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri (kushoto) akijaribu kumhadaa beki wa Yanga Oscar Joshua, wakati wa mchezo huo.
 Kocha wa Simba, Patrick Phir akiingia uwanjani.
Shabiki wa Simba.
Mashabiki wa Yanga.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo akiingia Uwanjani.
Waamuzi wa mchezo huo.
 Mashabiki wa Simba wakimzawadia pesa kipa wao, Manyika Peter baada ya kuokoa hatari nyingi langoni mwake. 

0 comments:

Post a Comment