Tuesday, October 21, 2014

 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden Experiece” yenye lengo la kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah
 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden Experiece” yenye lengo la kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kushoto kwa Pamela ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah na warembo wa Ndovu Special Malt.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah akionyesha namna ya kushiriki kampeni ya Ndovu Golden Experience kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden Experiece” yenye lengo la kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kulia kwa Fimbo ni Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli na warembo wa Ndovu Special Malt.


NDOVU Special Malt leo hii imezindua  kampeni yake kabambe ijulikanayo kama“Ndovu Golden Experience” ambapo itawazawadia watumiaji wa bia ya Ndovu zawadi kubwa ya kufanya matembezi ya utalii wa ndani nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari,  Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Bi. Pamela Kikuli alisema “ Utalii ni sekta muhimu sana katika nchi yetu hususani katika kukuza uchumi wa nchi ingawa  kuna watalii wengi sana kutoka nje ya nchi wenye muamko mkubwa kuliko watanzania.  Kwa sasa kampeni ya “Ndovu Golden Experience” imetoa fursa kwa Watanzania  kufanya utalii wa ndani ili  kujionea maajabu mazuri katika nchi yetu kwa kutembelea hifadhi za Seleous.
Bi. Pamela alienedela kufafanua na kusema, Kampeni hii ya bia ya Ndovu Special Malt inayojulikana kama “Ndovu Golden Experience” inategemea kuanza  katikati ya mwezi octoba mwaka huu ambapo kila wiki atapatikana mshindi mmoja atakayejipatia nafasi mbili za kutembelea mbuga za Selous, gharama zote zimelipiwa na bia ya Ndovu. Ili kushiriki katika shindano hili mtumiaji wa kinywaji cha Ndovu Special Malt anapaswa kutuma namba maalum ziilizowekwa chini ya kizibo cha bia ya Ndovu Special Mallt na kuzituma kwa SMS kwenda namba 15499 au kwa njia ya tovuti kupitia www.ndovuspecialmalt.com/goldenexperience.  Maelezo haya ya jinsi ya kushiriki yanapatikana pia kupitia nembo (lebo) ya nyumba ya bia ya Ndovu.

Meneja wa masoko wa  TBL Bw. Fimbo Butallah aliongeza  kwa kusema kuwa “ kampeni ya ‘Ndovu Golden Experinece’ ni muendelezo wa kampeni tuliyoanza nayo mwaka jana inayoujulikana kama Ndovu Defenders au Walinzi wa Tembo. Kampeni hii ilifanyika kupitia mitandao yetu ya kijamii ili kuwahamasisha na kusambaza elimu kwa Watanzania kuhusu ujangili dhidi ya Tembo, na mshindi wake pia alizawadiwa safari ya watu wawili ya kwenda kutembelea hifadhii zetu maarufu za wanyama za Selous. Na sasa hii kampeni ya ‘The Ndovu Golden Experience’ kwa mara nyingine inawapa nafasi watanzania ya kufanya utalii wa ndani na hapo tunaamini kuwa watapata motisha ya kulinda mali asili zetu, wakiwemo Tembo.

0 comments:

Post a Comment