Wednesday, October 8, 2014

 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelikindo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa mashindano ya Safari All Afrika Pool Championships yanayotarajiwa kuanza Octoba 16 mwaka huu katika Ukumbi wa Baudget Kunduchi jijini Dar es Salaam. .Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kutangaza uzamani wa mashindano ya Safari All Afrika Pool Championships yanayotarajiwa kuanza Octoba 16 mwaka huu katika Ukumbi wa Baudget Kunduchi jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelikindo.
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kudhamini mashindano ya mchezo wa Pool Afrika yajulikanayo kama “Safari All Africa Pool Championship 2014.”
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema, “ Kwa mara nyingine tena bia ya Safari Lager inashirikiana na Chama cha Pool nchini na Afrika kwa kudhamini  Mashindano ya Pool Afrika 2014 yatakayotambulika kwa “Safari All Afrika Pool Championships. Tunafanya hivyo ili kuhakikisha mchezo huu uanapanda na tunategemea timu yetu ya taifa itafanya vizuri zaidi ya matokeo ya mwaka jana.”
Shelukindo alisema TBL kupitia bia ya Safari Lager inawatakia kila la kheri timu ya Taifa kuanzia maandalizi mpaka mashindano yenyewe tukiamini Ubingwa unabaki Tanzania lakini pia aliwakumbusha ujumbe ambao tumekuwa tukiutumia kwa miaka kadhaa sasa wa “Play Pool Stay Cool” ambao hutukumbusha kuwa watulivu kila tuchezapo na kumaliza.
Nae Mwenyekiti wa Chama  cha Pool Taifa(TAPA), Isack Togocho aliishukuru TBL kwa mara nyingine tena kwa kudhamini mashindano hayo pamoja na timu ya Taifa ambayo kwa mara ya kwanza Tanzania tunakuwa waandaaji.
Alisema Togocho hii ni dhahili kuwa mchezo wa Pool sasa umekuwa Tanzania na kwa uandaaji huu tunaamini mwaka huu 2014 ushindi unabaki Tanzania.
Katibu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga alizitaja Nchi  zinazoshiriki mashindano ya Safari Pool Afrika kuwa ni Mabingwa watetezi wa mwaka jana, Zambia, Afrika Kusini, Malawi, Lesotho, Kenya, Uganda, na wenyeji Tanzania.
Kafwinga alisema mashindano yatafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 16,17 na 18,2014 katika Ukumbi wa Budget Kunduchi jijini Dar es Salaam.Timu kutoka katika nchi zote hizo tunatarajia zitaaanza kuwasili Octoba 15,2014.
Kuhusu timu ya Taifa ya Tanzania wanaendelea na mazoezi kwa pande zote mbili ya Wanaume na Wanawake lakini rasmi wataingia kambini Octoba 9,2014.
Meneja wa Bia ya Safari Lager alizitaja zawadi za washindi kuwa ni

ZAWADI
TIMU/NCHI
SINGLE’S
WANAUME
SINGL’S WANAWAKE
Mshindi wa Kwanza
5000$
2000$
1000$
Mshindi wa Pili
2000$
1000$
500$

0 comments:

Post a Comment