Saturday, October 18, 2014


 Baada ya kuonekana kuwa mrembo wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, amedanga kuhusu umri wake halali aliotakiwa kutaja ili Kamati ya mashindano ya Miss Tanzania iweze kumruhusu kushiriki mashindano hayo au la, wadau wa tasnia ya urembo wanaomfahamu kwa karibu mrembo huyo wamekuwa wakizidi kutoa baadhi ya vidhibitisho vya mrembo huyo vinavyoonyesha umri halisi ambao ni miaka 25 badala ya ile 18 aliyoitaja.
Aidha wadau hao wamezidi kwenda mbali zaidi kwa kuweka picha ya mrembo huyo inayoonyesha akiwa na mtoto wake jambo ambalo linazidi kuichanganya kamati ya mashindano hayo kwa kuona kuwa tayari huu ni mwaka wa tabu na kashfa kubwa kwao ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Japo inawezekana ilishawahi kutokea kwa warembo kudanganya kuhusu umri na kuwa na watoto, lakini haikuweza kuwa na kishindo na kuvuta hisia za wengi kama ilivyo kwa mrembo huyu wa 2014.
Kwa mawazo ya wadau wengi wa tasnia ya urembo, wamekuwa wakishauri kuwa ni bora kamati husika ikae chini na kuchukua maamuzi magumu ya kumvua taji hilo mrembo huyo na kumkabidhi mshindi wa pili, ili kuendelea kulinda heshima ya mashindano hayo ambayo kwa uhakika yanaelekea kupoteza mvuto na mwelekeo na hasa kutokana na kashfa kama hizi. 
Pichani ni moja ya picha zilizopostiwa na watu wa karibu wa mrembo huyo kuwa eti huyo aliye naye pichani ni mtoto wake, habari ambayo haina uhakika ila ni kwa mujibu wa mitandao.

PICHA ZA MISS TANZANIA 2014 KABLA HAJATIMIZA MIAKA 18....

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi.
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki zake wa mamtoni.
Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akiwa na baba yake, Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu wakati wa kutwaa taji.Picha Kwa Hisani ya GPL
.jump-link{ display:none }

0 comments:

Post a Comment