Sunday, November 2, 2014

Kagera Sugar na Yanga wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Na. Faustine Ruta/G. Sengo 
BUKOBA.
KLABU ya soka Dar es salaam Young Afrika imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.

Kipindi cha kwanza Timu zote mbili zilimaliza bila ya kufungana, Kipindi cha pili Kagera Sugar walitumia faida ya kucheza nyumbani na kufanikiwa kupata bao lililofungwa kiufundi na paul Ngwai na kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 na kuwaacha Yanga wakibaki na pointi zao 10 ambazo wamevuna katika michezo 6.


Katika mchezo huo Mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro baada ya kumpiga Kiwiko mchezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0, lakini kipindi cha Pili Kagera walifanya shambulizi kali na kuifunga Yanga bao 1-0 bao lililofungwa na Paul Ngwai na kuweza kutangulia kwa bao hilo 1-0 mpaka mwisho wa dakika 90. 
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya timu ya  Yanga kutoka Jijini dar es Salaam. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Kikosi cha Yanga.
Picha ya pamoja Timu kepteni na Waamuzi wa Mtanange 
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars'Martinus Ignatus 'Mart Nooij nae alikuwepo uwanjani kaitaba kujionea kipute hicho.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho kwenye Patashika na mchezaji wa Kagera Sugar.
Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akimtoka mchezaji wa kagera Sugar.
Andrey Coutinho akiwekwa chini ya Ulinzi na wachezaji wawili wa Kagera huku akionekana kuwazidi ujanja wenzake wa kagera.
Jaja juu kwa juu akigombea mpira wa kichwa.
Mchezaji wa kagera walipoteza muda mwingi kwa kujiangusha angusha wakivunga wameumia.
Nadir Haroub "Cannavaro" akisindikizwa nje ya Uwanja baada ya kuondolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Nadir Haroub "Cannavaro" akisindikizwa nje ya Uwanja baada ya kuondolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Tegete aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho na hapa alikuwa akichuana na Benjami Asukile wa Kagera Sugar.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange ndiye alikuwa kazini leo baada ya Kocha wao Jackson Mayanja kuwa nje kwenye Adhabu aliyopewa kwenye mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union.
Mchezaji wa Kagera chini tena dah..!!!
KOCHA Mkuu wa Yanga Marcio Maximo akimnyooshea kidole Mwamuzi wa kati baada ya mpira kumalizika Kaitaba Jioni hii Baada ya kuchapwa bao 1-0.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva na Marcio Maximo wote hawakuridhishwa na maamuzi ya refarii wa mchezo huo na hapa walikuwa wakilalama kwa wasimamizi wa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0.

0 comments:

Post a Comment