Monday, November 3, 2014

Vijana mbalimbali wameshiriki katika Timu za upigaji wa Makasia kwenye mashindano ya mitumbwi ya balimi yaliyofanyika leo Jumamosi 01-11-14 kwenye ziwa Victoria Mkoani Kagera wakichuana vikali kwenye michuano hiyo ambapo timu kwa upande wa wanaume iliibuka bingwa na kubadhiwa kitita cha Shilingi 900,000 na timu ya Wanawake kukabidhiwa kitita cha Sh 700,000.Wakina Mama wapiga Kasia nao wakiwa tayari kwa mashindano 

Tayari kwa Mashindano kuanza..
Wanaume Kazini! Washiriki wa Mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika kwenye Ziwa Victoria Bukoba.Wakina mama wakiwa Kazini Wadau mbalimbali walijitokeza kwa wingi katika Mashindano hayo ya Mitumbwi.Baadhi ya Washindi upande wa Kina Mama walioibuka KidedeaMama aliyeshinda akionesha zawadi ya pesa Wakina Mama wapiga Kasia walioshinda wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mtoto alishinda na kujinyakulia pesa. Baba nae aliibuka mshindi wa pili
Wapiga Kasia wakishangilia hapa baada ya Baba na Mtoto kushinda na kujinyakulia pesa taslim.Wanaume walioshinda wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi(katikati).

0 comments:

Post a Comment