Monday, November 17, 2014

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha...

Na Mwandishi wetu,Kagera.
KIKUNDI cha Wanaume  wapiga kasia cha Nichoraus Ngoroma Kisiwa cha Ukerewe kimeibuka na ubingwa katika fainali za mashindano yambio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya  Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa hicho kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Kapina Kagari ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Athumani Malemo ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Mashauri Saidi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Asante Robert, Ladsilaus Musimu, Benedicto Aniseti, Gervas Kulwa, Simon Fundi na  Silvari Sasieli.
Upande wa Wanawake kikundi cha Muhate Mwocha kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza.Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Mlanzi Mussa ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Joyce Makalu ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Beatrice Kalomba  ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Pili Masitu, Adventina Elias, Jesca Jose, Veronica Machumu,Juliana Petro na Maria Mabagara.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha  kwanza alitoa shukrani kwa Kampuni ya bia nchini(TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo na kuwaomba waendelee kudhamini kwani yanaleta hamasa umoja na udugu kati yetu kuiachilia mbali afya na kipato kinachopatikana kama zawadi mara baada ya mashindano.
Tesha alisema washindi waliopatikana wakaiwakilishe vyema Ukerewe na wahakikishe wanarudi na ushindi na wale ambao hawakupata nafasi ya kushinda wajiandae kwa mashindano mengine mwakani.
Tesha alimaliza kwa kuwaomba zawadi walizopewa wakazitumie kwab maendeleo yao kwani huo ni mtaji tocha kwa mtu anayeweza kujishughulisha.
Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika  Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.

Washindi wa kwanza wa mbio za makasia wa Kisiwa cha ukerewe kikundi cha Nichoraus Ngoroma wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki.

0 comments:

Post a Comment