Wednesday, November 5, 2014Na Josephat Lukaza

Tasnia ya Filamu nchini imeanza kukua japo kwa mwendo wa kinyonga huku tukianza kuona baadhi ya wasanii katika tasnia hii wakianza kunufaika japo sio sana lakini tofauti na zamani. Leo Katika Filamu nitaongelea swala la Part 1 na 2 katika Filamu zetu za nyumbani.
Swala la Part 1 na 2 hapa nchini imekuwa ndio fasheni kutokana na watengenezaji, wasambazaji au wasanii wenyewe kuleta filamu ikiwa kwenye part 1 na 2 huku kiukweli ikiwa ni wizi kwa Mtanzania ambae anaenda kununua filamu hiyo, Mtanzania anaweza kuipenda filamu flani na akawa na uwezo wa kuinunua hiyo hiyo moja lakini utakuwa filamu hiyo story yake imekatwa mara mbili huku kipande cha pili kikiandikwa part 2 je huu sio wizi?

Endapo mtanzania huyu hatokuwa na pesa ya kununua part 2 maana yake ni kwamba amedhulumiwa haki yake na wewe uliyeikata story na kuitengenesha kuwa sehemu wakati story ni moja.

Ifikie hatua Watanzania nao wajue kuwa Kununua Filamu yenye part 1 na 2 ni wizi ambao wao wenyewe wanaibiwa kimacho macho na wafahamu kuwa Kununua filamu ya part 1 na 2 ni kununua story moja kwenye DVD mbili. Ndio maana tunasema Part 1 na 2 ni wizi kwa mtazamaji.

Filamu za Part 1 na 2 ni filamu ambazo kwanza hazina ubora wa kimataifa kwasababu ili filamu iweze kushinda tuzo labda nje ya nchi cha kwanza ni Filamu hiyo kuwa na Ubora wa Picha, Story na vilevile iwe moja ambayo story yake imekamilika.nk.

Leo hii Tanzania ikitoka filamu ambayo haina part 1 na 2 basi watanzania wachache ambao wanajua nini maana ya filamu ndio huweza kununua filamu hiyo kwasababu filamu yenye Part 1 na 2 ukiiangalia Utakugundua kuwa kuna baadhi ya vipande katika Filamu hizo havina umuhimu wa kuwepo lakini vinawekwa ili kuongeza muda tu na kuifanya part 1 iwe ndefu kidogo ili story iendelee part 2 VIpande hivyo ambavyo unaweza kukuta havina ulazima wa kuwepo ni kama kipande ambacho kinaweza kumuonyesha mshiriki wa filamu hiyo anatembea muda mrefu takribani dakika moja nzima inamuonyesha anatembea au anafungua Geti, au watu wanaongea weee kipande hikohiko kimoja sasa hii yote ni kwaajili ya Kujazia tu ili wakate story iendelee part 2...

Inatakiwa kufikia mahali sasa Watanzania tuinuke na tufungue macho sasa maana kununua filamu yenye part 1 na 2 ni wizi tunaojitakia wenyewe kutokana na kwamba tunakubali kununua story moja katika DVD Mbili.

Swala la Part 1 na 2 imekuwa mtindo sasa kwa wasanii wetu kutoa story moja ambayo ilitakiwa kuchukua lisaa limoja na dakika 20 basi Part 1 utaiona inachukua dakika 50 huku vipande vya filamu hiyo vingi vikiwa havina umuhimu wa kuwepo lakini msanii anaviweka ili kujazia muda tu katika filamu yake huku part 2 ikiwa fupi.

Mfano wa Filamu nyingi tu za Kitanzania ambazo zimeshinda tuzo huko marekani ni filamu ambazo Hazina Part 2 ni Part 1 tu... Kutokana na Uhalisia kuwa Ni vigumu sana kulibadilisha Soko lilivyo lakini Kampuni ya PRoin Promotions imejivunia kuwa ni Kampuni ambayo imeshaanza kuleta mabadiliko katika Tasnia hiyo huku Baadhi ya wasanii na wasambazaji wengine kuanza kufuata mtindo wake wa Kupokea Filamu yenye Part 1 tu... Proin Promotions inasema kwamba yenye hata kama story ikiwa na Masaa kumi basi itakuwa katika DVD moja kuliko kumuibia Mtanzania ambae anahitaji kupata kile anachostahili kwa bei nzuri huku akiwa haangaishwi katika Kununua Story moja katika DVD mbili.

Mpaka sasa tayari kuna baadhi ya Wasambazi na wasanii wameanza kufuata mtindo huo wa kutoa Sehemu moja ya filamu tu huku wengine wakijitahidi kuweka Dvd Mbili katika Kasha moja. Hili kwa Proin wanajivunia kutokana na watu kuanza kuzoea mfumo wao walioingia nao Sokoni.

Na Vilevile filamu za kitanzania nyingi zimeshaingia kwenye mfumo huo wa part 1 na 2 huku baadhi ya wasanii au wasambazaji wakikataa kupokea filamu yenye part 1 na 2.

Kampuni ya Proin Promotions ni moja ya Kampuni ya Usambazaji, utengenezaji wa filamu nchini ambayo iliingia sokoni na Staili ya kukataa Part 1 na 2, huku filamu zake zote ni sehemu moja tu. Kampuni hiyo inayofanya vizuri katika soko ikiwa na filamu ya MDUNDIKO ambayo ilichukua tuzo nchini Marekani kutokana na ubora wa Story yake ambayo haikuwa na part 2, Kampuni hii ya Proin Promotions ambayo mpaka sasa imeshatoa Filamu takribani 16 na zote zikiwa zimefanya vizuri sokoni huku Filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ikiendelea kukimbiza Sokoni kwa kununuliwa Kwa Wingi kutokana na Ubora wake na ni filamu ambayo imechezwa na Lulu, Lina na Mama Kanumba. Proin Promotions ni Kampuni ambayo kwanza imeweza kuleta mapinduzi katika Tasnia hii ya Filamu kwa kutonunua hatimiliki ya Msanii wa filamu husika.

Hivi karibuni Kampuni ya Proin Promotions Ltd itaingiza sokoni filamu yake Mpya nyingine iitwayo NEVER GIVE UP iliyochezwa na Slim, Hashim Kambi, Irene Paul na Staa wa Filamu Kutoka Nchini Ghana ajulikanaye kama VAN VICKER. Filamu hii itakuwa sokoni kuanzia tarehe 10 November 2014 huku ikiaminika kufanya vizuri zaidi sokoni.

Mpaka Sasa Kampuni ya Proin Promotions imeshatoa Filamu kama, Foolish Age, Long Time, Figo, Fedheha, Kitendawili, Siri Ya Mtungi Season 1 na Season 2, Kimbulu,Network, Sunshine, Mdundiko, I Love Mwanza, Joti Sanduku la Babu, Family Curse, Nitadumu Nae, huku Mapenzi ya Mungu na Kigodoro zikiwa ni filamu zinazofanya Vizuri mpaka sasa Sokoni.

Usikose nakala yako halisi ya Filamu moja wapo kati ya Hizo huku Ukiendelea kusubiri kwa hamu Filamu ya NEVER GIVE UP

0 comments:

Post a Comment