Tuesday, January 20, 2015


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifungua semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini,ufunguzi huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kuwashirikisha Viongzi wa ngazi za juu wa serikali ya Mapinduzi  wakiwemo Mawaziri,Naibu Mawaziri,Makatibu Wakuu,Naibu Makatibu Wakuu na Watendaji wengine.
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifurahia jambo wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
 Mshauri wa Rais Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa alipokuwa akielezea dhamira nzima ya semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa wajumbe wa Semina hiyo na kuwatambulisha Watoa mada katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo ambapo Mwenyekiti wa Semina hiyo akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri na watendaji wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia kwa makini wakati zilipokuwa zikitolewa mada katika semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Mtaalam kutoka Malaysia Dk.Idris Jala Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuupia Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa utafutaji ufumbuzi wa matatizo kwa njia za vikao vya wataalam mbali mbali wa(maabara) ya Malaysia (PEMANDU) akitoa mada katika semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayoshuhulikia utafiti katika ufumbuzi wa matekeo makubwa na ya haraka Bw.Omari Issa kutoka Tanzania Bara wakati alipokuwa akitoa mada yake wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa Mwenyekiti wa Semina hiyo. Picha na Ikulu.

0 comments:

Post a Comment