Friday, January 9, 2015


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi  sita iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa na matapeli katika jimbo lake la Chalinze.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi
 Mkuu wa Miradi wa Mkoa wa Pwani wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi umeme utakavyosambazwa katika Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine Jimbo la Chalinze.
 Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru mbunge kwa ahadi mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika kijiji hicho.
 Ridhiwani akibadilishana mawazo na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Fukayosi Jimbo la Chalinze.
 Mwenyekiti mstaafu wa Kata ya Fukayosi,Adam Masoud  akimuomba Mbunge Ridhiwani kuhikisha anaweka miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya katika Kijiji cha Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi.
 Mkazi wa Kijiji cha Mkenge, Khamis Mwanga akielezea kero ya barabara ya Mwavi hadi Mkenge ambayo alidai inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho hivyo kumtaka Ridhiwani awasaidia kuijenge barabara hiyo ili iweze kupitika bila matatizo katika vipindi vyote. Ridhiwani aliwajibu kuwa tayari barabara hiyo imepata mkandarasi anayetarajia kuanza kazi katika siku chache zijazo.
 Katibu wa CCM Tawi la Mkenge, Omar Seleman akimuomba Mbge Ridhiwani asaidie kumalizia ujenzi wa msikiti wa Mkenge, Ombi ambalo alilikubali na kuahidi kupaua kwa gharama zake.
 Ridhiwani akijibu maswali mbalimbali ya wananchi wakati wa mkutano katika Kijiji cha Mkenge
 Ridhiwani akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Mkenge ambao ameahidi kuchangia mabati na mbao za kupaua jengo hilo la ibada.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Fukayosi, Olnjurie Marigwa akihtubia katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi
 Masoud Fundikira akimuomba Mbunge wao Ridhiwan, anzishe mashindano ya mpira wa miguu kuwania kikombe cha Ridhiwani Cup ili kuendeleza michezo katika jimbo hilo. Ridhiwani alilikubali ombi hilo kwa kuanzia kutoa misaada ya mipira na jezi katika kila timu ya kata za jimbo hilo.
 Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Mwavi ambapo aliahidi kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la alilogawiwa Mkorea ili kijiji cha mwwavi kipate haki.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Kombo Kamote, akiwafunda viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwavi waliochaguliwa hivi karibuni ili wawatendee haki wananchi.
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kidomole, ambapo aliwajia juu anaowaita matapeli wanaouza ardhi katika Jimbo la Chalinze bila kufuata sheria na utaratibu. Alisema kuwa hayuko tayari kuona hata heka moja ya jimbo hilo ikikuzwa bila utaratibu.
Ridhiwani akiagana na Meya wa  Morogoro, Amir Nondo ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo hilo la Chalinze.
Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Msata, Rehema Mno akielezea kwa wananchi jinsi alivyoshiriki kutatua kero za wananchi katika Kata ya Kiwangwa., Ridhiwani akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kiwangwa, Yahaya Ramadhani wakati wa mkutano huo Sehemu ya umati uliohudhuria katika mkutano huo Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwaambia viongozi wa Tanesco kuhakikisha wana peleka haraka umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Kiwangwa Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chalinze, Julius Doyi akiwaambia wananchi wa Kiwangwa kuwa umeme utaingia hapo mwezi huu. Meneja wa Mamlaka ya Usafi wa Maji Safi na Taka wa Chalinze,Injinia Christer Mchomba akielezea kwa wananchi mikakati mbalimbali ya kuharakisha upatikanaji wa maji katika Kata ya Kiwangwa. Ridhiwani akaimkabidhi Bondia Idd Pialali gloves 20 kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa ngumi katika Kata ya Kiwangwa Ridhiwani akimkabidhi mpira mmoja wa wa manahodha wa timu mbalimbali katika Kata ya Kiwangwa kwa ajili ya kuendeleza soka katika kata hiyo.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
RIDHOIWANI KIKWETE AAHIDI KUTATUA TATIZO LA UMEME,MAJI KIWANGWA, CHALINZE Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ, Aloyce Mayunga (kushoto) alipokwenda kukagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kikazi ya katika Kata ya Kiwangwa, wilayani Chalinze, Pwani leo.Aliwataka wajenzi hao kujenga maabara hayo kwa kuzingatia viwango. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo, Saleh Mpimbwi. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakandarasi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ wanaojenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kuagua miradi ya maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita iliyopita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Ridhiwani akinyoosha juu kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kijiji cha Masugulu ambaye amehamia CCM katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwitemo Kata ya Kiwangwa leo Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji cha Mwitemo Sehemu ya akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani Kikwete akihutubia katika Kitongoji cha Magogoni, Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa. Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa. Msanii kiongozi wa Kikundi cha sanaa cha Chanzala akifanya maajabu yake wakati mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa, akifungua rasmi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka jana. Mkazi wa Kiwangwa Shabani Dume akiuliza swali kwa kumtaka Mbunge Ridhiwani asaidie kuwepo dampo katika Kijiji cha Kiwangwa Kassim Makelele wa Kata ya Kiwangwa akimuomba Mbunge Ridhiwani kununua Ambulance kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kiwangwa Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Msata, Rehema Mno akielezea kwa wananchi jinsi alivyoshiriki kutatua kero za wananchi katika Kata ya Kiwangwa., Ridhiwani akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kiwangwa, Yahaya Ramadhani wakati wa mkutano huo Sehemu ya umati uliohudhuria katika mkutano huo Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwaambia viongozi wa Tanesco kuhakikisha wana peleka haraka umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Kiwangwa Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chalinze, Julius Doyi akiwaambia wananchi wa Kiwangwa kuwa umeme utaingia hapo mwezi huu. Meneja wa Mamlaka ya Usafi wa Maji Safi na Taka wa Chalinze,Injinia Christer Mchomba akielezea kwa wananchi mikakati mbalimbali ya kuharakisha upatikanaji wa maji katika Kata ya Kiwangwa. Ridhiwani akaimkabidhi Bondia Idd Pialali gloves 20 kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa ngumi katika Kata ya Kiwangwa Ridhiwani akimkabidhi mpira mmoja wa wa manahodha wa timu mbalimbali katika Kata ya Kiwangwa kwa ajili ya kuendeleza soka katika kata hiyo.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

0 comments:

Post a Comment